Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis akiangalia sehemu ya Mradi wa Ufugaji Samaki katika Kijiji cha Mapofu wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya Miradi ya kurejesha Ardhi iliyoharibika kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi na kuongeza Usalama wa Chakula ukihusisha Ujenzi wa Matuta ya kuzuia maji ya Bahari kuingia katika mashamba ya mpunga, upandaji wa miti ya mikoko, Matumizi ya Majiko Banifu na Ukaguzi wa Visima vya Maji ambapo mradi huo pia unatekelezwa katika wilaya za Magu, Nzega, Mkalama na Kondoa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Micheweni,Mgeni Khatib Yahya akitoa maelezo juu ya mradi wa ufugaji wa Samaki katika Kijiji cha Mapofu wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya Miradi ya kurejesha Ardhi iliyoharibika kutokana na mabadiliko ya Tabia ambapo mradi huo pia unatekelezwa katika wilaya hiyo
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni,Mgeni Khatib Yahya(kulia) wakitembea kuelekea sehemu ya Mradi wa Ufugaji Samaki katika Kijiji cha Mapofu wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya Miradi ya kurejesha Ardhi iliyoharibika kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi na kuongeza Usalama wa Chakula ukihusisha Ujenzi wa Matuta ya kuzuia maji ya Bahari kuingia katika mashamba ya mpunga, upandaji wa miti ya mikoko, Matumizi ya Majiko Banifu na Ukaguzi wa Visima vya Maji ambapo mradi huo pia unatekelezwa katika wilaya za Magu, Nzega, Mkalama na Kondoa.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis akitoka kukagua kibanda cha mbuzi kinachoonekan pichani katika Shehia ya Kiuyu Mbuyuni wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya Miradi ya kurejesha Ardhi iliyoharibika kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi na kuongeza Usalama wa Chakula.Picha Ofisi ya Makamu wa Rais
Na Mwandishi Wetu,Pemba
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis ametoa muda wa wiki mbili kwa Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba kukamilisha taratibu za zabuni na ununuzi wa Pampu, Mashine za Umeme wa Jua na Matanki ya kuhifadhia maji ili huduma ya maji safi iweze kuwafikia wananchi wa kijiji cha maziwa ng’ombe.
Ametoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua Miradi ya kurejesha Ardhi iliyoharibika kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi na kuongeza Usalama wa Chakula ukihusisha Ujenzi wa Matuta ya kuzuia maji ya Bahari kuingia katika mashamba ya mpunga, upandaji wa miti ya mikoko, Matumizi ya Majiko Banifu na Ukaguzi wa Visima vya Maji ambapo mradi huo pia unatekelezwa katika wilaya za Magu, Nzega, Mkalama na Kondoa ambapo gharama yake kwa ujumla ni Shilingi Bilioni Kumi na Tano.
‘Kuna mambo tukiyafanya tunapoteza Imani kwa wananchi,waanchi hawa wanataka maji waanze kutumia sasa nakupa muda wa wiki mbili mkakae hivyo vikao vya zabuni na mkamilishe huo mchakato,sisi wote hapa tunaendeleza na kutekeleza azma ya marais wetu wote wawili,Rais Dkt. Samia na Dkt.Hussein Mwinyi ambao wamekua wakipeleka huduma kwa wananchi sasa sisi wengine hatuna sababu ya kuchelewesha huduma mbalimbali Kwenda kwa wananchi na tayari fedha ya mradi huu ishatoka,kwanini wananchi hawapati maji.’amesema Khamis
Wakizungumza wakati wa ziara hiyo wananchi wa Kijiji cha Maziwa Ng’ombe wamesema wamekua wakipata maji kila mwisho wa mwezi hali inayowapelekea kutumia gharama kubwa na umbali mrefu kufuata maji huku gharama hizo kubwa zikiendelea kuwasababishia hali ngumu ya Maisha huku wakimuomba Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Khamis Hamza Khamis kutatua kero hiyo kupitia mradi wa kurejesha Ardhi iliyoharibika kutokana na mabadiliko ya Tabia Nchi na kuongeza Usalama wa Chakula ambapo katika Kijiji chao watanufaika na mradi wa uchimbwaji wa visima.
Mradi huo wa visima hivyo vya maji ambavyo vipo katika Kijiji cha Maziwa Ng’ombe vipo katika hatua ya zabuni kwa ajili ya ufungaji wa pampu,mashine za umeme wa sola na matanki ya maji ambayo naibu Waziri Khamis ametoa muda wa wiki mbili ili mchakato huo wa zabuni ukamilike.