Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mwantumu Mahiza akimwagilia maji mara baada ya kupanda mti katika Shule ya Sekondari Ilazo Extension jijini Dodoma Oktoba 03, 2023 wakati wa Siku ya Kwanza ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Vicknes Mayao akimwagilia maji mara baada ya kupanda mtu katika Shule ya Sekondari Ilazo Extension jijinip Dodoma Oktoba 03, 2023 wakati wa Siku ya Kwanza ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Baadhi ya wadau kutoka Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakishiriki kupanda miti katika Shule ya Sekondari Ilazo Extension jijini Dodoma Oktoba 03, 2023 wakati wa Siku ya Kwanza ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Mwantumu Mahiza na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Vickness Mayao wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kupanda miti katika Shule ya Sekondari Ilazo Extension jijini Dodoma Oktoba 03, 2023 wakati wa Siku ya Kwanza ya Jukwaa la Mwaka la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WMJJWM)
Na.Alex Sonna-DODOMA
MWENYEKITI wa Bodi ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mhe.Mwantumu Mahiza,amezitaka taasisi mbalimbali nchini kuhakikisha zinatunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Mhe.Mahiza ametoa maelekezo hayo leo Oktoba 3,2023 jwakati wa zoezi la upandaji miti liliofanyika Shule ya Sekondari Ilazo Extension jijini Dodoma.
Mhe.Mwantumu amesema jamii inatakiwa kuhamasika katika utunzaji wa mazingira ikiwepo kupata hewa safi pamoja na Mvua zakutosha kuzalisha chakula.
“Tumekuja hapa kupanda miti kwa lengo kuhihamasisha jamii suala la kutunza mazingira sio la Serikali au Kikundi cha watu fulani ni jukumu letu sote tujitoe tutunze mazingira yetu” amesema Mhe.Mwantumu
Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Green Eco Tanzania Stanley Shibuda amesema Shirika hilo linahamasisha upandaji wa miti kwa nchi nzima na kwasasa limeanza kwa Mkoa wa Dodoma kwa lengo la kupanda miti 1500 na mpaka sasa wamehamaisha kupanda miti 300.