Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak (wa pili mbele) akisikiliza maelezo kuhusu kilimo cha mbogamboga kwa umwagiliaji wa matone katika Kijiji cha Melela alipotembelea Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) katika Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak (wa pili mbele) akitembelea shamba la nyanya katika Kijiji cha Melela alipotembelea Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) katika Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak akifurahia nyanya alipotembelea shamba la zao hilo katika Kijiji cha Melela alipotembelea Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) katika Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak akizungumza wakati alipotembelea lambo la kuvunia maji ya mvua katika Kijiji cha Melela alipotembelea Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) katika Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak akikagua kilimo cha mbogamboga zinazolishwa kwa umwagiliaji wa kisima kirefu kilichochimbwa katika Kijiji cha Mingo alipotembelea Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) katika Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak akiwa katika picha ya pamoja na wanakikundi cha kilimo cha mbogamboga na watumishi wa Serikali katika Kijiji cha Mingo alipotembelea Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) unaotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) katika Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
………………………………
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Dkt. Omar Dadi Shajak ametoa wito kwa Halmashauri zilizonufaika na Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia Vijijini (EBARR) kuusimamia vyema ili uwe endelevu.
Ametoa wito huo alipofanya ziara ya kukagua mradi wa EBARR unaotekeleza na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) katika Halmashauri ya Mvomero mkoani Morogoro.
Katika ziara hiyo amekagua lambo na kilimo cha mbogamboga kwa umwagiliaji wa matone na shamba darasa la uyoga, ujenzi wa kiwanda kidogo cha bidhaa za ngozi, kisima kirefu na vitalu nyumba katika Kijiji cha Mingo.
Akionesha kuridhishwa na utelezaji wa mradi, Dkt. Shajak amesema kwa vile kuna ukomo wa muda wa utekelezaji miradi, ni muhimu kutambua ni namna gani shughuli zitakuwa na muendelezo.
“Sisi kule kwetu ni kisiwa, uvuvi na utalii ni shughuli kuu na kupitia mradi huu vikundi vya uvuvi vilioatiwa boti kupitia EBARR na wao wakajiongeza siku ambayo hawavui wanasafirisha watalii kwenda kwenye visiwa kutalii na kupata fedha ambazo zimewasadiai kununua boti nyingine, hayo ndio mategemeo yetu,” amesema.
Aidha, Dkt. Shajak amesema nia ya Serikali ya kuwapelekea wananchi miradi ni kuwasaidia waweze kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kufanya shughuli za kujiongezea kipato na wakati huo wanatunza mazingira.
Hivyo amesema kuwa shughuli zinazofanyika kupitia mradi huo ziwe chachu ya kutoa fursa zikiwemo za kilimo na kupunguza au kuondoa kabisa changamoto kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Linno Mwageni ameishukuru Serikali kwa jitihada za kuboresha Maisha ya wananchi.
Amesema kupitia Mradi wa EBARR wananchi walioshindwa kufanya shughuli za kujipatia kipato zikiwemo kilimo na ufugaji kutokana na changamoto ya ukame sasa wamepata fursa ya kujiajiri.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Melela Mhe. Mecklaud Lugata amesema miradi hii imewasaidia kuepukana na kufanya shughuli zinazochangia kuharibika kwa mazingira zikiwemo ukataji wa miti.
Amesema wananchi watajipatia kipato kutokana na kujishughulisha na kilimo cha mbogamboga pamoja na kiwanda kidogo cha bidhaa za Ngozi ambacho kiko katika hatua za ujenzi.
diwani
“Tunaishukuru sana Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kutuletea Mradi wa EBARR ambao umetuletea maendeleo na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi kwani matumzi ya misitu kiholela yamepungua,” amesema.
Ziara Dkt. Shajak akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Bi. Farhat Mbarouk na Mratibu wa Mradi wa EBARR Bw. Alawi Hija ina lengo la kujifunza utekelezaji wa shughuli za mradi kwa upande wa Tanzania Bara.
Mradi unatekelezwa pia katika Halmashauri ya Mpwapwa (Dodoma), Simanjiro (Manyara), Kishapu (Shinyanga) na Kaskazini ‘A’ Unguja kwa lengo la kuwawezesha wananchi kufanya shughuli za kujipatia kipato huku wakihifadhi mazingira.