Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya mradi wa umeme wa Rusumo, unaotekelezwa na nchi tatu za Tanzania, Rwanda na Burundi ambao hadi sasa umekamilika kwa asilimia 99.7 leo Tarehe 3/10/2023.
Mradi huo unatarajiwa kuzalisha megawati 80 na kila nchi itapata megawati 27 katika gridi yake.
Kukamilika kwa mradi huu kutarahisisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za umeme hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Kagera, Geita na Kigoma.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Prof. Mark Mwandosya amesema, kukamilika kwa mradi huo wa kihistoria kutaleta ongezeko la umeme kwa nchi zote tatu na kuchochea uwekezaji katika viwanda na kukuza uchumi.