Timu ya Kamba wanawake ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimenyana katika moja ya Michezo yao.
Michuano Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali na Mikoa (SHIMIWI) imezidi kurindima katika viunga vya mji wa Iringa ambapo Timu za Kamba za Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( ME na KE )zimeendeleza ubabe wao kwa timu katika Makundi yao.
Katika michezo ya leo Oktoba 01,2023 timu ya Kamba ya Uchaguzi wanaume wamewahenyesha na kuchukua alama mbili kutoka kwa timu ya Kamba kutoka Tume ya Haki za Binadamu.
Mchezo huo ambao awali ulikua unaonekana kuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na aina ya wachezaji waliopo lakini ulikuwa mwepesi kwa miamba ya Uchaguzi.
Katika mchezo mwingi timu ya wanawake wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imefanikiwa kuingia katika hatua ya 16 bora hii ni baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Timu ya Mahakama.
Baada ya matokeo hayo sasa timu ya wanaume wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imebakiza michezo miwili dhidi ya Timu ya Kamba kutoka Ikulu na Timu ya Kamba kutoka TARURA.
Kundi la H la Kamba wanaume lina timu za Ikulu,NEC, TARURA,Tume ya Haki za Binadamu,Pamoja na Maliasili huku upande wa Kundi A timu ya Kamba wanawake kulikuwa na timu za NEC, Tume ya Utumishi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi pamoja na Mahakama.