DAR ES SALAAM
Viongozi wa Chama cha Ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Jeshi la Polisi, usalama wa raia saccos – URA SACCOS wametakiwa kujipanga vyema kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mfumo wa kidijitali kwa wananchama ili kuondoa uwezekano wa kujitokeza kwa changamoto wakati wa matumizi ya mfumo huo.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (mb) wakati wa uzinduzi rasmi wa mfumo wa kidijitali wa huduma za kifedha ambapo amesema mfumo huo utaongeza uwazi, kupunguza gharama na kuwafikia wanachama kwa urahisi.
Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura amesema kuwa hadi sasa URA SACCOS imefanikiwa kutoa huduma bora za kifedha kwa wanachama wake ikiwemo mikopo nafuu na kuboresha ustawi wa askari, watumishi raia na familia zao.
Aidha, IGP Camillus Wambura Ametoa rai kwa ambao bado hawajajiunga na mfuko huo kwani URA SACCOS ni mkombozi wa Maisha kwa watumishi wote waliopo ndani ya Jeshi la Polisi.