Na John Walter-Manyara
Hatimaye ligi inayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini Daniel Sillo (SILLO CUP 2023) kata ya Madunga imefikia tamati kwa Madunga FC kuwa mabingwa.
Lengo la Mashindano hayo ni kutafuta vijana wenye vipaji na kuanzisha timu ya wilaya itakayoshiriki ligi daraja la Kwanza (championship), ligi daraja la pili (SDL) na hata ligi kuu.
Kwa sasa wilaya ya Babati ina uwanja mzuri wa kisasa (Kwaraa) wenye viwango vinavyohitajika na shirikisho la soka la Kimataifa hivyo ni fursa kwa timu zitazofanya vyema.
Mamia ya wakazi wa Madunga walifurika uwanja wa njia panda kushuhudia fainali Kali iliyowaacha Kijiwe Star vichwa chini kwa kichapo cha chuma 4-1 kutoka kwa ya Madunga FC.
Baada ya kivumbi hiki Cha Sillo Cup, Kata 25 zitazokuwa zimepatikana zitachuana katika ligi ya tarafa kutafuta timu kwenye kila tarafa.
Babati Vijijini ina vijiji 102, tarafa nne za Bashnet yenye kata 10 Arri, Ayalagaya, Dabil, Dareda,Bashnet, Ufana,Secheda, Qameyu,Madunga na Nar.
Tarafa ya Babati yenye kata nne za Galapo,Mamire, Endakiso na Qash.
Tarafa ya Gorowa yenye kata Tano ambazo ni Ayasanda,Boay, Gidas,Duru,Riroda.
Tarafa nyingine ni Mbugwe yenye jumla ya kata sita za Magugu, Mwada,Kisangaji, Nkaiti, Magara na Kiru.