Mbunge wa Jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku Musukuma (kulia aliyeshika barua) akizungumza na Wavuvi wa Mwaro wa Makatani Kata ya Nkome wilayani Geita ambao wanalalamikia kutozwa faini kinyume na utaratibu.
…………………………………………………..
Na Victor Bariety Geita
MBUNGE wa
Jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku Musukuma ameuagiza uongozi wa BMU
Mwaro wa Makatani uliopo Kata ya Nkome
wilayani Geita kurejesha fedha zaidi ya Sh.400, 000 walizochukua kwa baadhi ya
wavuvi wa mwaro huo ambazo waliwatoza kama faini ya kuvua dagaa wakati wa giza
kinyume cha utaratibu.
Mbunge Musukuma ametoa agizo hilo alipofanya
ziara ya kushitukiza kwenye mwaro huo kisha kuzungumza na wavuvi wa eneo hilo
ambapo bila kumung’unya maneno wavuvi hao walimweleza mbunge wao kuwa uongozi
wa BMU kata hiyo wamekuwa wakiwanyanyasa Kwa kuwatoza faini zisizo rafiki
pasipo hata kuwapatia risti za malipo hayo.
“Mheshimiwa mbunge bora umekuja yaani baadhi ya viongoz wa BMU hapa makatani
wanatunyanyasa sana na wamekuwa wakituzuia kuvua dagaa majira ya giza lakini
pia wanapotukamata wanatutoza faini ya shilingi elfu hamsini na hatupewi risiti
ya malipo hayo” alisema Mussa Juma huku akishangiliwa na wavuvi wenzake na
kuongeza mfano juzi tumekamatwa na tumetozwa faini ya Sh.50,000 kila mmoja na hatukupewa
risti”
Kufuatia malalamiko hayo Mbunge Musukuma alitaka
kupata ufafanuzi kutoka Kwa uongozi Wa kijiji hicho ña kuelezwa KUWA agizo hilo
limetoka Kwa uongozi Wa Halmashauri hiyo lengo likiwa ni kuokoa mazalia ya
samaki”
Mheshimiwa mbunge siyo kwamba sisi tumejiamulia
kuwakamata hawa wavuvi ni agizo kutaka Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na lengo
ni kufanya samaki wazaliane”alisema Mtendaji wa Kata ya Nkome John Nzari.
Hata hivyo baada ya maelezo hayo kutoka kwa
mtendaji, Musukuma alipitia barua iliyotoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo
inayoelekeza utekelezaji wa agizo hilo alihoji iwapo kwenye barua hiyo
wameagizwa kuwatoza faini wavuvi hao pasipo kupatiwa risti lakini nakupata
majibu yanayojitosheleza.
“Ni kweli hii barua imewaelekeza kukamata
wavuvi wanaovua dagaa nyakati za Giza lakini ni wapi ambapo imeelekeza muwatoze
faini pasipo kuwapatia risti?” alihoji
Musukuma
kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa BNU kata hiyo
Ntuzu Emmanuel alijitetea kuwa walikuwa na mpango wa kuwaita wavuvi hao ili
wawapatie risti zao uteteziambao pia uligonga mwamba kwa mbunge huyo na kuamuru
pesa hiyo irejeshwe haraka Kwa wavuvi hao na iwe mwanzo na mwisho kuwatoza
wavuvi hao pesa zao pasipo kuwapatia risti.
“Sasa nisikikizeni naomba pesa uliyochukua
Kwa wavuvi muirejeshe Mara moja na iwe mwanzo na mwisho kuwatoza faini pasipo
kuwapatia risti, mnasikia nyie wavuvi msikubali kutoa hela bila kupewa risti
hata serikali inasisitiza unapofanya malipo ya aina yoyote ile dai risti”
alisema mbunge Musukuma huku akipigiwa makofi
Kufuatia Hali hiyo uongozi huo Wa bmu
ulimhakikishia Mbunge pesa yote watairejesha na kwamba suala hilo
halitajitokeza tena.
Katika hatua nyingine wavuvi hao walimtaka mbunge
huyo kuondoka na mtendaji wa kijiji hicho Salum Mussa Kapami kwa madai amekuwa
ni mungu mtu.
“Mheshimiwa mbunge uondoke na mtendaji wa
kijiji amekuwa amekuwa Mungu mtu
tunaomba uondoke naye” alisema Geradi masaga huku akishangiliwa na wavuvi
wenzake
Aidha, akijibu malalamiko hayo Musukuma alimtaka
mtendaji huyo kujibu hoja za wavuvi hao na kudai KUWA anasingiziwa
“Ninakuomba ujirekebishe ukiendelea hivyo
nitaongea na mkurugenzi akuondoe maana wameshaondoka watendaji wengi sana hapa
ambao hawawezi kutatua kero za wananchi” alisema Musukuma.