Na John Walter-Manyara
Mbunge wa jimbo la Babati mjini na naibu waziri wa katiba na sheria Mhe. Pauline Gekul leo amekutana na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Maji na Nishati [Ewura CCC] Mkoa wa Manyara na kuitaka taasisi hiyo kushiriki katika mikutano ya wananchi kwa lengo la kutatua na kusikiliza kero za wananchi.
Mhe. Gekul ametoa wito huo ili kuongeza juhudi za kutoa elimu na kusikiliza kero za wananchi wanazopata kuhusiana na huduma za maji,Nishati ya Umeme na Gesi kupitia mikutano ya hadhara ili wananchi waitambue taasisi hiyo
Kwa upande wake Afisa Msaidizi Huduma kwa wateja na utawala kutoka
Ewura CCC -Manyara bi Neema Nnko amesema lengo la kukutana na mbunge huyo ni kuitambulisha taasisi hiyo na kushirikiana na mbunge huyo ili kutatua kero za wananchi.
Aidha ameongeza Kuwa [EWURA CCC] ipo kwaajili ya kuwatetea watumiaji wa huduma za maji, umeme na gesi kama iwapo wamekutana na changamoto zozote na kutoridhishwa na huduma hizo.