Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF imesema imesaini mikataba yakupeleka Mawasiliano vijijini ambapo kata zaidi ya 1900 nchini zitafikiwa na huduma za Mawasiliano kwa kujengewa minara katika maeneo ambayo huduma hizo zilikuwa hazipatikani.
Aidha inaelezwa kuwa mara baada ya mradi huo kukamilika Watanzania zaidi ya milioni 15 watapata huduma hiyo ya Mawasiliano katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa UCSAF Bi.Justina Mashiba Wilayani Handeni Mkoani Tanga katika kijiji cha Msomera wakati akielezea utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo kwa ujumla na kazi ambayo UCSAF imefanya ya kuboresha Mawasiliano na kupeleka vifaa vya Tehama katika kijiji hicho.
“Jukumu ambalo tunalo sisi UCSAF ni kupeleka Mawasiliano kwa wote na mpaka sasa tumefikia asilimia 90 bado asilimia 10 tu kuweza kukamilisha zoezi la upelekaji wa huduma hizo. Kipekee zaidi niwashukuru watoa huduma za Mawasiliano wote nchini kwa ambavyo wamekuwa wakishirikiana na Mfuko huu kwa kutoa huduma kwa wananchi”
“Sisi tunakwenda maeneo ambayo ni magumu kufikika Serikali iliamua kuwatoa ndugu zetu ambao walikuwa wanaishi Ngorongoro na kuwaleta katika kijiji cha Msomera wilayani Handeni
Sisi tumefanya miradi mitatu tumejenga minara hapa kwa kushirikiana na TTCL na wao wameweka vifaa vyao pale”amesema Mashiba
Amesema katika kijiji hicho usikivu wa huduma za mitandao unapatikana kwa mitandao yote kwa kasi ya 4G na hilo likiwa ni moja kati ya juhudi za Serikali katika kuhahakisha huduma za Mawasiliano zinapatikana kwa wananchi wote.
Akizungumzia kuhusu kijiji cha mkababu ambacho watu watakuja kuishi wanaendelea kipeleka hudum hapo na mradi huo upo katika huduma za mwishoambapo mpaka amesema mpaka watakapofika watakuta huduma za Mawasiliano zimekamilika.
“Pia kuhusu TEHAMA kwa wanafunzi wa jamii ya kimasai amesema shule ya msingi Samia Suluhu Hassan ni moja ya shule zilizonufaika kwa kupata huduma za darasani za tehama kwa watoto” amesema Mashiba