Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (kushoto), akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Hassan Babu (katikati), alipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambapo anafanya ziara ya siku mbili mkoani humo kusikiliza changamoto mbalimbali wanazopitia wafanyabiashara na kuhamasisha matumizi sahihi ya mashine za Kieletroniki (EFD). Kulia ni Mbunge wa Moshi Mjini, Bw. Priscus Tarimo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Kilimanjaro, katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambapo anafanya ziara ya siku mbili mkoani humo kusikiliza changamoto mbalimbali wanazopitia wafanyabiashara na kuhamasisha matumizi sahihi ya mashine za Kieletroniki (EFD).
Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Tixon Tuyangine Nzunda (kulia), na Kamishna Msaidizi wa Uchambuzi wa Sera wa Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja (katikati), wakiwa katika kikao cha Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) (hayupo pichani) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Hassan Babu (hayupo pichani), katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Hassan Babu, akimkaribisha Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb),wakati wa kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo, katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, mjini Moshi.