Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga -Bombo Dkt Naima Yusuf
Na Oscar Assenga,Tanga.
Ni ukweli usiopingika kwamba huduma za Afya ni muhimu kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya jamii katika harakati za kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wao na Taifa kwa ujumla.
Jamii isipopata huduma nzuri za afya inaweza kushindwa kutimiza ipasavyo majukumu yake hususani katika shughuli zake za kila siku za kujiletea maendeleo na hivyo kupelekea kuwa tegemezi.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga –Bombo ni miongoni mwa Hospitali za Rufaa hapa nchini ambazo zimenufaika na uwekezaji mkubwa wa Bilioni 3.5 ambao umefanya na Rais Dkt Samia Suluhu hapa nchini katika kuhakikisha huduma za afya zinaimarika.
Anaeleza Serikali imewasaidia kujenga jengo la wagonjwa mahututi ,magonjwa ya dharura pamoja na kutanua sehemu ya matibabu ikiwemo ya vijana wanaotumia dawa za kulevya (Methadone) huku miradi mingine ikitarajiwa kujengwa kwenye Hospitali hiyo.
Dkt Naima anaeleza kwamba pia kuna mradi wa damu salama ambapo watakuwa wanapataa huduma ya damu salama kwenye mkoa na hospitali ya Rufaa ambao utakuwa ni mkombozi kwa wananchi.
Anaeleza kuhusu vifaa tiba anasema Serikali awamu ya sita imewasaidia kununua vifaa tiba vingi vya uchunguzi mpaka vya kutolea matibabu ambavyo ni CT Scan ambayo imeleta huduma ya uchunguzi,vifaa vya dharura pamoja na kuweka fedha kwenye mafunzo ,ujenzi kwa ajili ya watalaamu.
“Uwekezaji huo umegharimu sh Bilioni 3.5 kwa ujumla ambao umefanywa chini ya mwaka mmoja na hivyo huduma zimepanuka Bombo wagonjwa wengi waliokuwa wakipata rufaa sasa hivi wanapata huduma hapa hapa hayo ni mafanikio makubwa sana”Anasema Dkt Naima
“Tulikuwa tunatoa rufaa wagonjwa 50 mpaka 60 kwa wiki mbili lakini kwa sasa ni chini ya rufaa 25 kwa wiki mbili hayo ni mafanikio makubwa sana na wananchi wa Tanga wanamshukuru sana Rais Dkt Samia Suluhu kwa uwekezaji huo mkubwa”Anasema Dkt Naima
Anasema wameweza kupanua huduma za uchujaji wa damu na huduma za watoto njiti ambao wanahudumiwa hapo hapo kwa ajili ya vifaa na kupanua huduma za dharura ambazo kwa sasa zimeimarika.
Hata hivyo anasema wameweza pia kupanua huduma ya mkojo kutokana na kwamba unapofikia uzee wapo wanaopata shida ya tezi dume huduma sasa inapatikana ikiwemo zile za macho,pua koo na masikio na meno na huduma mahututi.
“Nikisema huduma za mahututi na dharura tumeweza kufufua wagonjwa waliokuja bila mapigo ya moyo kama watano ambayo hiyo ingekuwa haiwezekani bila kuwa na vifaa tiba msaada huo ambao tumesaidiwa na Serikali utusaidia kufanikisha hayo”anasema
Kuhusu Ajira. Dkt Naima anaendelea kuishukuru Serikali ya awamu sita kwenye kuwasaidia kuwapelekea waajiriwa wapya 50 kutokana na kwamba hiyo imesaidia kuleta huduma kwenye maeneo walioyapanua kuwa na madaktari ,manesi pamojà na wataalumu katika kada mbalimbali.
“Nakumbuka nilivyoanza hapa Hospitali ya Rufaa ya Bombo mwaka 2008 Bombo kulikuwa na madaktari bingwa chini ya 11 na waliokuwa wanatoa huduma walikuwa wanne tu leo tuna madaktari bingwa 21 kwa kweli ni hii ni pongezi kubwa sana kwake Rais Dkt Samia Suluhu na Waziri wetu wa Afya Ummy Mwalumu”alisema Dkt Naima
Alisema leo wameona umuhimu wa kuwapeleka madaktari na wameweka bajeti ya kuwaongeze ujuzi madaktari bingwa watano kufikia kwenye Ubingwa Bobezi wanasubiri bajeti ikipita waende kwenye mafunzo na warudi kutoa huduma hapo.
Kuhusu upatikanaji wa Dawa
Dkt Naima anasema kuhusu suala la upatikanaji wa dawa wameongezewa bajeti ya kununua dawa na mfumo wa upatikanaji wa dawa umekuwa mzuri mwanzoni walikuwa wanapata shida kutoka MSD .
Alisema kwa maana dawa nyingi zilikuwa hazipatikana lakini sasa hivi alikuwa amekaa na Meneja MSD na wameona ongezeko lilivyokuwa sasa hivi imefikia asilimia 57 na dawa nyingi watapa MSD na mlolongo wa upatikanaji wa dawa utapungua.
Hata hivyo Dkt Naima anasema hospitali hiyo inatambua kuwa na madaktari bingwa 21 sio sahihi kubaki tu Hospitalini kuna wananchi wengi wanashindwa kuja hospitaklini Tanga kutokana na umbali wa maeneo ya wilayani hivyo kwakutambua hilo wanakwenda kutoa huduma kwenye hospitali hizo ikiwemo kuwafundisha wataalamu walipo kwa hiyo kwa mwaka wanafanya mara nne na wanajaribu kwenda wilaya zote za Tanga.
Anaeleza kwamba Bombo Hospitali ni miongoni mwa Hospitali za Rufaa 28 nchini ambapo kwa sasa wanajivunia kwenye umahiri wa Plastic Surgery mradi ambao ulianza 2011 kuna madatari wanatoka nchini Ujerumaani kwenye hospitali yao na kufika kwenye Hospitali hiyo ya Bombo wanafanya kliniki za ubobezi za Plastic Surgery.
Anasema hiyo imesaidia watu wengi hapa nchini ambao wakati wa kliniki hizo wamekwa wakijitokeza kupata huduma hiyo na wamechukua hatua baada ya Waziri kuona kuna umihumu wa kuendelea nayo hapa hivyo wameanzisha Programu ya Plastic Surgery unaitwa Tazzy Plastic ambao utakuwa unatoa huduma ndani ya Hospitali.
Dkt Naima anasema huduma hiyo itakwenda sambamba na kuanzisha program ya kufundisha madaktari ili kuweza kupata madaktari bobezi katika eneo hilo na madaktari wawili wanakwenda kusoma wapo na ushirikiana na Muhas na Muhimbili na watakachokifanya ni kufanya eneo la Umahiri katika Urekebishaji Viungo(Plastic Surgery) hapa nchini .
Anasema unapoongelea urekebishaji wa viungo sio ya kufanya mtu awe mrembo ila ni watu waliozaliwa mfano mdomo au pua haijaka vizuri au walioungua na mikono yao haijakaa vizuri wanachofanya wanamuweka vizuri ili waweze kufanya kazi kama kawaida na kuirudisha ngozi na kufanya kidonda kukaa vizuri kwa hiyo ni huduma kama hizo.