Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana,akizungumza na Menejimenti ya Tume ya kurekebisha sheria Tanzania mara baada ya kutembelea Ofisi hiyo na kupokea taarifa mbili za namna Ofisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake leo Septemba 22,2023 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana katika Ofisi ya Tume ya kurekebisha sheria Tanzania kutembelea Ofisi hiyo na kupokea taarifa mbili za namna Ofisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake leo Septemba 22,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Jaji Mstaafu Januari Msoffe,akiwasilisha taarifa kwa Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana,mara baada ya kutembela Ofisi ya Tume ya kurekebisha sheria Tanzania leo Septemba 22,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Tume hiyo, Griffin Mwakapeje,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana katika Ofisi ya Tume ya kurekebisha sheria Tanzania kutembelea Ofisi hiyo na kupokea taarifa mbili za namna Ofisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake leo Septemba 22,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya Menejimenti wakimsikiliza Waziri wa Katiba na Sheria Balozi Dkt. Pindi Chana (hayupo pichani) wakati ,akizungumza baada ya kutembelea Ofisi ya Tume ya kurekebisha sheria Tanzania mara leo Septemba 22,2023 jijini Dodoma.
Na.Gideon Gregory-DODOMA
Waziri wa Katiba na Sheria balozi Dkt. Pindi Chana amewapongeza viongozi wa Dini nchini kwa juhudi zao za kuendelea kupambana na vitendo vya ukatili na kuahidi kuwa,Serikali itaendelea kushirikiana nao vyema katika kuhakikisha vinatokomezwa katika maeneo yote nchini.
Waziri Chana ameyaeleza hayo leo Septemba 22,2023 Jijini Dodoma alipotembelea Ofisi za Tume ya kurekebisha sheria Tanzania na kupokea taarifa mbili za namna Ofisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.
Amesema katika mashirikiano hayo wanapaswa kuzingatia vyema sheria na taratibu walizojiwekea na wakishindwa kufanya hivyo watakuwa wanafanya jambo ambalo sio sawa na wale waliopewa dhamana ya kusimamia eneo la katiba na sheria watimize wajibu wao.
“Tutaendelea kuwakumbusha watanzania, tutaendelea kutoa elimu tuzingatie taratibu fikiri sehemu ambazo mmejiwekea taratibu lakini mwingine anafanya kazi mwingine anaiba mali alizotafuta mwenzake yaani anaenda anachukua tu hiyo sio sawa, mwingine anapita tu mwingene anachukua panga anamtwanga tu hii haiwezekani tuna taratibu zetu,”amesema Dkt. Chana.
Aidha ameongeza kuwa hawatovumilia watu wanaovunja sheria na kuvikumbusha vyombo vya ulinzi maali popote ambapo watu hawataki kufuatia utaratibu ambao umewekwa wasisite kutoa taarifa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa katiba na sheria Jaji Mstaafu January Msofe amesema kuwa utafiti kuhusu makosa ya maadili ulibaini kuwa makosa hayo yamekuwa yakiongezeka nchini ambapo mwaka 2021 jumla ya makosa 7601 ya kubaka na kurawiti yaliripotiwa na mwaka 2022 makosa 8413 yaliripotiwa.
“Hata hivyo kesi zinazofunguliwa mahakamani ni chache kuliko zile zinazotolewa taarifa katika vituo vya polisi matharani katika kipindi cha 2021/22 na 2022/23 ofisi ya taifa ya mashtaka ilifungua mahakamani kesi 2980 na 4294 mtawalia za makosa dhidi ya maadili yakiwemo ya ukatili, kubaka, kujaribu kabaka, kurawiti, na kujaribu kurawiti,”amesema Jaji Mstaafu Msofe.
Jaji Mstaafu Msofe ameongeza kuwa taarifa zionesha kuwa kuna kesi kubwa za makosa dhidi ya maadili ambazo hazijaripotiwa katika vyombo husika.
Naye katibu Mtendaji wa tume hiyo Griffini Mwakapeje amesema kuwa jumla ya ripoti zilizowasilishwa serikalini ni 56 na kuongeza kuwa katika kufanya hivyo tume inaweza kufanya uchunguzi wa sheria yoyote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lengo la kuiendeleza.
“Kwa kuelekezwa na wewe Waziri au mwanasheria mkuu wa serikali tume inaweza kutoa ushauri wa kisheria au msaada wa kisheria pale inapobidi na inapotekeleza majuku haya tume inaweza kufanya mashirikiano na taasisi nyingine za serikali na binafsi halafu na kutoa taarifa zake,”amesema Mwakapeje.