WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene,akizungumza wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 21 hadi 22 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene amewataka waajiri nchini kuhakikisha wanasimamia na kuimarisha uzingatiaji wa maadili ya viongozi wa umma na watumishi wa Umma.
Hayo ameyasema hayo leo Septemba 21,2023 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora Waziri Simbachawene amesema Ofisi yake itaendelea kushirikiana na Mamlaka simamizi za maadili ya kitaaluma kutoa ushauri wa kitaalamu pale itakapohitajika
“Kikao hiki cha wadau katika usimamizi wa maadili ni kikao muhimu kinachosaidia nchi katika kuimarisha usimamizi wa rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma. Hivyo, nichukue fursa hii kuwataka waajiri nchini kuhakikisha wanasimamia na kuimarisha uzingatiaji wa Maadili ya Viongozi wa Umma na Watumishi wa Umma,”amesema Waziri Simbachawene.
Pia,Wadau wa Maadili ikiwemo Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma kuendelea kushirikiana na OR- MUUUB kujenga uelewa wa Miongozo mipya ya usimamizi wa maadili kwa watumishi iliyotolewa na ofisi hii.
“Mamlaka za nidhamu kuendelea kufuatilia na kuchukua kwa wakati hatua stahiki dhidi ya vitendo vya ukiukwaji wa Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma,”amesema Waziri Simbachawene.
Vilevile,kufanya tathmini ya utekelezaji wa Maazimio na Mpango Kazi wa Kikao kilichopita ili kubaini mafanikio na changamoto zilijitokeza katika utekelezaji wa maazimio hayo na kuja na mapendekezo ambayo yatasaidia Serikali kuimarisha uadilifu katika Utumishi wa Umma.
“Kuhimiza matumizi ya Serikali Mtandao ambayo imeonesha mafanikio makubwa katika kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa Maadili katika Utumishi wa Umma,”amesema Waziri Simbachawene.
Waziri Simbachawene amesema malengo mahsusi ya kikao kazi hicho ni kubadilishana uzoefu na taarifa zinazojumuisha mafanikio na changamoto za usimamizi wa maadili katika Utumishi wa Umma.
Pia,kubuni na kuweka mikakati ya kuimarisha Maadili ya Utumishi wa Umma na kitaaluma kama sehemu ya kutatua changamoto.
“Natoa rai kwenu, kwamba mikakati hiyo iandaliwe kwa lengo la kukuza Uwajibikaji na Usikivu wa Umma kama moja ya msingi wa Utawala Bora.
Amesema wajibu wa kusimamia Maadili ya Watumishi wa Umma na Utawala Bora katika Utumishi wa Umma ni suala mtambuka ambalo liko chini ya Ofisi ya Rais,Utumishi na Utawala Bora kwa kusaidiana na Taasisi Simamizi za Maadili na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma.
“Hivyo, kwa kuzingatia dhamana mliyopewa katika kusimamia Maadili, mnapaswa kuendelea kushirikiana na kuwekeza katika mikakati ambayo itachangia kukuza Uwajibikaji na Usikivu wa watoa huduma kwa wananchi hususani katika maeneo yanayoigusa jamii moja kwa moja au kulalamikiwa mara kwa mara,”amesema Waziri Simbachawene.
Ameyataja maeneo hayo ni pamoja na sekta ya afya, elimu, ujenzi, ardhi, manunuzi na ugavi.
Amesema Azma ya Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuona Utumishi wa Umma wenye usikivu na uwajibikaji wa hiari kwa ustawi kwa wananchi wa Tanzania.
“Hivyo, ili kuendana na maono hayo ya Mhe. Rais, Ofisi yangu imekuwa ikitumia njia mbalimbali ikiwemo kuweka mifumo ya uwajibikaji na kuzishirikisha Taasisi Simamizi za Maadili na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma katika ukuzaji na ufuatiliaji wa uzingatiaji wa Maadili katika Utumishi wa Umma.
Amesema ushirikiano huo, unaiwezesha Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kufahamu hali halisi ya uadilifu katika Utumishi wa Umma na kuchukua hatua stahiki.
Amesema Matarajio hayo yatafikiwa iwapo ushikiano utatafsiriwa kwa kuandaa, kuhuisha na kutoa Miongozo mbalimbali ya kusimamia Uadilifu katika Utumishi wa Umma.
Pia,kujenga uelewa wa miongozo hiyo kwa umma; na kufanya ufuatiliaji wa uzingatiaji wa Maadili kwa mujibu wa miongozo.
“Na kama mnavyofahamu hivi karibuni ofisi yangu ilihuisha Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma za mwaka 2005 na Mwongozo wa Ushughulikiaji wa Malalamiko ya Wananchi wa mwaka 2012.
Amesema ili kutokomeza malalamiko ambayo yanaelekezwa katika Taasisi za Umma, Taasisi Simamizi za Maadili na Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma wanapaswa kufanyia kazi maeneo mawili.
Ameyataja maeneo hayo ni kutoa elimu kwa wanataaluma ili wazingatie miiko ya taaluma zao na mafunzo ya Maadili kwa watumishi wa umma ili wazingatie Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia Maadili ya utendaji kazi na yale ya kitaaluma.
Pia, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na Taratibu ambapo Mamlaka Simamizi za Maadili ya Kitaaluma zinapaswa kusimamia na kuchukua hatua stahiki kwa wakati kwa wale wanaokiuka Maadili ya taaluma zao.
Vilevile, kushughulikia kwa wakati malalamiko yanayotokana na Uvunjifu wa Maadili kwa lengo la kuendelea kujenga imani kwa wananchi na kuongeza uwajibikaji na usikivu.
Kwa upande wa Taasisi Simamizi za Maadili na Utawala Bora, wanatakiwa kufuatilia uzingatiaji wa Maadili ya Viongozi na Watumishi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazoongoza taasisi.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejmenti ya utumishi wa umma na utawala bora,Bw. Xavier Daudi,amesema lengo la kikao hicho ni kubadilishana uzoefu na kuweza kushirikiana ili kuweza kufahamu changamoto walizonazo na kama ni mafanikio na masuala mapya yanayojitiokeza katika utumishi wa umma lakini lengo letu ni kurudisha maadili tunayotarajia katika utumishi wa umma.
”Kikao hiki tutapokea mada mbalimbali hivyo naamini mada zitakazowasilishwa sio tu zitaleta chachu katika majadiliano lakini pia zitasaidia kuleta suluhisho na kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali za maadili zinazotukabili.”amesema Bw.Daudi
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene,akizungumza wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 21 hadi 22 jijini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejmenti ya utumishi wa umma na utawala bora,Bw. Xavier Daudi,akielezea lengo la kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 21 hadi 22 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene (hayupo pichani) wakati akifungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 21 hadi 22 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene,akiwakabidhi Viongozi mbalimbali Kitabu cha Kanuni za Maadili mara baada ya kufungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 21 hadi 22 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe.George Simbachawene,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Septemba 21 hadi 22 jijini Dodoma.