Mwalimu Mkuu wa Almadrasatul-Shaafiiyya Islamiya Hussein Idd Salim akizungumza na uongozi wa Skuli ya Trifonia Academy walipofika Chuoni hapo katika ziara yao kuelekea kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake
Walimu na Wanafunzi wa Skuli ya Trifonia Academy wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Madrasatu Shaafiiyya Islamiya wakati walopowatembelea ikiwa ni miongoni mwa shughuli za kusherehekea miaka 25 tangu kuanzishwa kwa skuli hiyo.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO
Na Rahma Khamisi Maelezo
Wadau mbalimbali chini wameombwa kuunga mkono jitihada zinazochukuliwa na walimu wa madarasa ili kuwasaidia wanafunzi katika kukuza elimu ya kumtambua mola wao.
Wito huo umetolewa huko Madrasati Shafaia Mwanakwerekwe na Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Trifonia Idd Hussein Idd wakati alipotembelea Madrasa hiyo ikiwa ni shamrshamra za kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.
Amesema wadau wengi wamejikita katika kusaidia mambo mengine ya kijamii na kuziacha Madrasa bila ya kuzipitia jambo ambalo si la kufurahisha kwani elimu zinazotolewa katika madrasa hizo ni muhimu na zinasaidia kuwakuza watoto hao katika maadili mema na kuwajenga kiimani .
“Naiomba jamii na wadau wa elimu kujitokeza kuzisaidia Madrasa ambazo mazingira yake hayako vizuri ili kupata radhi za Mola wetu,”alisisitiza Mwenyekiti.
Nae Mwlimu Mkuu wa Skuli ya Trifonia Protas Bernado Nikodem amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza , kuangalia mazingira ya madrasa hiyo na kusaidia panapohitaji msaada ili kuweka muzingira rafiki ya kujifuniza kwa wanafunzi hao .
Aidha amefahamisha kuwa kazi ya waalimu wa Madasa ni kazi ya wiito, hivyo ipo haja ya kuwaunga mkono kwa kuwapa mashirikiano ya hali ya juu ili kuendeleza kufanya kazi hiyo .
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Madarasa hiyo Hussein Idd Salim amesema madrasa hiyo ni mbovu kwa muda mrefu sasa hali inayowakosesha amani na utulivu wa kusoma hasa katika kipindi cha mvua.
Aidha ameiomba Serikali kuzingatia muda waasomo kwani wanafunzi wengi wanatoroka Madrasa kwa kisingizio cha kwenda masomo ya ziada (tution).
Katika hatua nyingine Mwalimu Mkuu amewaomba wazazi na walezi kuongeza ushikiano kwani baadhi yao wanashindwa kuwasilisha michango kwa wakati jambo linapolekea kurudisha nyuma maenedeleo ya Madrasa hiyo.
Hata hivyo amepongeza na kuushukuru Uongozi wa Skuli ya Trifonia kwa kufika katika madrasa yao na kuwataka Skuli nyengine kuiga mfano huo ili kukuza elimu za vijana.
Matembezi hayo ni muendelezo wa ziara ya skuli ya Trifonia kupeleka mrejesho kwa jamii ikiwa ni shamrashamra za kutimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake.