NJOMBE
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete ametoa wito kwa wazazi ambao watoto wao wanakwenda kuanza kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba katika halmashauri hiyo kuwapunguzia kiwango chai ili kuepusha watoto kupata usumbufu wa kutoka nje mara kwa mara wakati wakiwa ndani ya chumba cha mtihani.
Mpete ametoa wito huo wakati wanafunzi wakianza akizungumza kufanya mitihani yao.
“Watoto ni vema wapunguze kiwango cha kunywa chai,kama mtoto amezoea kunywa vikombe viwili basi ni vizuri kipindi hiki cha mitihani anywe nusu kikombe na pia kiwango cha maji nacho wapunguze kwasababu kibofu kitajaa mkojo na mtoto atalazimika kutoka mara kwa mara”amesema Mpete
Aidha Mpete ametoa wito kwa wazazi kuacha kuwagombeza au kuwaadhibu watoto kwa kipindi hiki ili waweze kuwa vizuri kiakili na kufaulu mitihani yao.
Vile vile amepiga marufuku wazazi kuanza kushinikiza watoto kufeli kwa matarajio ya kuwapeleka kufanya kazi badara yake waache watoto wasome kwa kuwa Njombe sio kiwanda cha kuzalisha wafanyakazi za nyumbani.
“Kuna wazazi wengine wanataka watoto wao wakimaliza tu darasa la saba kama ni wasichana wanataka wakwe ni mahouse girl na kama ni wavulana wakwe house boy,niwaomba sana wazazi kama elimu ni ufunguo wa maisha ni jukumu la mzazi kuhakikisha mtoto anafanya mtihani na anafaulu”aliongeza Mpete
Jumla ya wanafunzi 4871 wameanza kufanya mitihani yao ya darasa la saba kuanzia hapo kesho September 13 mwaka 2023 katika halmashauri ya mji wa Njombe ambapo halmashauri hiyo imejipanga vema katika maandalizi hayo huku wakitajia kufanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani kitaifa.