Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bunare Daniel akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi hiyo namna ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma (NeST) wakati wa kikao cha wafanyakazi hao hivi karibuni katika ukumbi wa Taasisi hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Bunare Daniel akimuelekeza kwa vitendo namna ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma (NeST) Afisa Uuguzi wa Taasisi hiyo Salma Wibonela wakati wa kikao cha wafanyakazi hao hivi karibuni katika ukumbi wa Taasisi hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakisikiliza wakati wa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo mpya wa kielektroniki wa manunuzi ya Umma (NeST) hivi karibuni katika ukumbi wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Picha na: JKCI