Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Nyasa tarehe 07.09.2023, imetambulisha mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya Tsh Bilioni 4.1utakaotatua kero ya maji safi na Salama katika Kata 2 za Kilosa na Mbamba bay Wilayani Nyasa.
Mradi huo umetambulishwa katika mikutano ya Hadhara wenye lengo la kuwashirikisha wananchi, ili waweze kushirikiana na Mkandarasi atakayetekeleza Mradi, Mkutano iliyofanyika katika Kata ya Ofisi ya Mtendaji wa Kijiji Cha Nangombo Kata ya Kilosa na kuhudhuriwa na wananchi na Viongozi wa Chama na Serikali.
Akizungumza katika Mkutano, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mh.Filberto Sanga, amemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi, kuhakikisha anajenga mradi kwa ubora na kwa wakati na kuhakikisha maji yanatoka, na kuwa Mradi endelevu kwa kuwa Serikali inalengo la kutatua kero ya maji, hivyo fedha za Serikali ziendane na thamani halisi ya Mradi. Pia amewataka wananchi kutoa ushirikiano katika Mradi na kulinda na kutunza Vyanzo vya maji.
“Ninakutaka Mkandarasi utakayetekeleza Mradi huu kuhakikisha kuwa unajenga kwa ubora na maji yanatoka, na kuwa mradi endelevu kwa kuwa Serikali inalenga kutatua kero ya maji, hivyo fedha za Serikali ziendane na thamani halisi ya Mradi,na wananchi naomba tushiriki kikamilifu Ujenzi wa mradi huu Kwa kuwa ni wetu na unalengo la kutatua kero ya maji katika mji wetu wa Mbamba bay Kwa kuwa tulikuwa na miradi midogo midogo
Awali akitoa Taarifa ya Miradi hiyo Meneja wa RUWASA Wilayani Nyasa mhandisi Masoud Samila,amemtambulisha Mkandarasi Peritus Exim Private ltd kutoka Dar es salaam ndie atakayetekeleza mradi huu na amesema,wamejipanga kimkakati kusimamia na kutekeleza miradi hiyo ili iweze kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi kwa wananchi.
Amesema Mradi huu unalenga kuhudumia wananchi wapatao 13,323 na amevitaja vijiji vitakavyonufaika na mradi huu ni Nangombo, Likwilu, Ruhekei, kilosa na Mbamba bay.
Ameongeza kuwa shughuli zitakazofanyika ni Ujenzi wa Tego la maji,ujenzi wa Tanki lenye ujazo wa Lita milioni Moja(1,000,000),ununuzi wa Bomba, ulazaji wa mabomba km 4.9 ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji na Miradi hiyo itatekelezwa kwa kipindi cha miezi sita na unataraji