Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akipitia nyaraka mbalimbali wakati wa Kikao cha majumuisho kwa ujumbe wa Tanzania kilichofanyika kwenye bustani ya Cresta Mowana Hotel, kabla ya kuhudhuria Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu unaofanyika Mjini Kasare -Botswana. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na kulia ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bi. Sauda Msemo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akiongoza Kikao cha majumuisho kilichofanyika katika bustani ya Cresta Mowana hotel Mjini Kasane – Botswana, kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), katikati (walioketi), akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka Tanzania uliohudhuria Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu, unaofanyika katika hotel ya Cresta Mowana, Kasane – Botswana. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb),akifuatilia baadhi ya matukio katika ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hotel ya Cresta Mowana, nchini Botswana.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akifuatilia baadhi ya matukio katika ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu, unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano uliopo katika Hotel ya Cresta Mowana, nchini Botswana.
Baadhi ya ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), wakifuatilia baadhi ya matukio katika ufunguzi wa Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu, unaofanyika katika Hoteli ya Cresta Mowana, nchini Botswana.
(Picha na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha-Botswana)
Na Ramadhani Kissimba, Botswana
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 23 wa Baraza la Mawaziri na Maafisa Waandamizi wa Umoja wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika wa Kudhibiti Utakasishaji Fedha Haramu (Eastern and Southern Africa Anti Money Laundering Group (ESAAMLG), unaofanyika katika mji wa Kasare, nchini Botswana, kuanzia tarehe 8 -9 Septemba, 2023.
Mkutano huo wa siku mbili, pamoja na mambo mengine, utajikita katika kujadili mifumo na mbinu mbalimbali za udhibiti wa fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi katika nchi wanachama wa ESAAMLG.
Aidha, Mkutano huo ambao ulitanguliwa na vikao vya Makatibu Wakuu wa nchi wanachama, ulijadili taarifa ya utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya Tathmini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu Mwamba, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Dkt. Khatibu Kazungu, walishiriki.