Na Sophia Kingimali
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kuwa Afrika haihitaji kusaidiwa Bali inahitaji haki yake ya keki ya Dunia ili kuweza kutumia rasilimali za pamoja katika kuleta maendeleo ya nchi.
Hayo ameyasema Leo Septemba 8 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tathmini ya mkutano wa Mifumo ya chakula(AGRF) uliofanyika kwa siku nne jijini Dar es salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere JNICC.
Amesema mkutano huo umekua na manufaa makubwa Kwani umefungua njia za kuboresha miundombinu ya kuboresha kilimo nchini.
“Nipende kuwashikuru watu wote waliofanikisha mkutano huu wa AGRF hasa AGRA umekua mkutano wenye faida sana Kwa nchi hasa kwenye sekta ya kilimo “amesema Bashe
Amesema jumla ya Dola za kimarekani bilioni 550 zimepatikana Kwa ajili ya kuboresha kilimo Kwa kuendeleza miradi ya vijana na wanawake.
Amesema miradi hiyo inepangwa kutekelezwa Kwa kipindi Cha miaka mitatu Hadi mitano.
” Ili kutanua sekta ya kilimo lazima tuwekeze kwenye miundombinu Bora ya kilimo Kwa kuhakikisha mkulima anapata Mbegu Bora lakini pia miundombinu ya maji”ameongeza Bashe.
Mkutano wa jukwaa la mifumo ya chakula AGRF umekua na manufaa makubwa Kwani wakulima na wafanyabiashara za kilimo nchini 3000 wamehudhulia huku washiriki kutoka nje wakiwa 2000 ambapo lengo la mkutano limefikiwa Kwani ilikua lengo kubwa kupata pesa na ushirikiano Kwa ajili ya kuboresha sekta ya kilimo ili kufikia malengo ya nchi kuwa na chakula Cha kutosha na kulisha Dunia ili dhima ya kilimo biashara ifikiwe Kwa vitendo.