Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mhe. Edward Ole Lekaita wakati wa Mkutano wa 12 wa Kikao cha 6 Bungeni jijini Dodoma.
…
WATUMISHI wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa , wametakiwa wabadilike katika utendaji wao na wasiishi kwa mazoea.
Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe.Mohammed Mchengerwa alipokuwa akichangia Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, Jason Rweikiza kuhusu matokeo ya uchambuzi wa sheria ndogo zilizowasilishwa Bungeni katika Mkutano wa 10 Septemba 20, 2022 na Mkutano wa 11 wa Bunge Novemba 7, 2022.
Pia taarifa hiyo imetoa matokeo ya uchambuzi wa taarifa za utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu dosari na hitilafu za sheria ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Nane na Mkutano wa Tisa wa Bunge.
“Tumepokea mapendekezo ya Kamati, naomba watumishi wenzangu tuache utendaji wa kimazoea, “ amesema na kuhakikisha kuwa sheria na kanuni vitaendana na Katiba.
Pia amesema atahakikisha sheria na kanuni mbalimbali zinaboreshwa ili kulinda, kutetea maslahi ya wananchi.