Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, Mhe. Simai Sadiki wakati Kamati hiyo ilipopewa Semina ya Shughuli zinazofanywa na Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, kuhusu Shughuli zinazofanywa na Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), wakati kamati hiyo ilipokutana jijini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo, Mhe. Simai Sadiki.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo wakifuatilia Semina ya Shughuli zinazofanywa na Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), iliyowasilishwa kwao na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Bw. Nelson Mlali, jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), Nelson Mlali akifafanua jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo (hawapo pichani), kuhusu mapato yanayokusanywa na wakala huo wakati Kamati hiyo ilipopewa Semina ya Shughuli za Shirika hilo, jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC), Nahodha Mussa Mandia akifafanua jambo kwa Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo kuhusu shughuli zinazofanywa na Shirika hilo wakati Kamati hiyo ilipopewa Semina ya Shughuli za Shirika hilo, jijini Dodoma mwishoni mwa wiki.
PICHA NA WIZARA YA UCHUKUZI