Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akizungumza wakati wa akizindua zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya katika wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akizindua zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, uzinduzi uliofanyika wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Sehemu ya washiriki wa uzinduzi wa zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya uliofanyika Bagamoyo mkoa wa Pwani .
Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Stela Tullo akizungumza kwenye uzinduzi wa zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya uliofanyika wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani .
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga akisikiliza moja ya shauri katika Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Bagamoyo mara baada ya kuzindua zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri ya ardhi katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya.
Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Nyumba na Wilaya wilaya ya Kibaha na Bagamoyo Mhe. Mathias Lung’wecha akiendesha shauri la ardhi lililohudhuriwa na Katibu Mkuu wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga. Wengine katika picha ni Wazee wa Baraza.
Baadhi ya Wadaawa wakioongozwa na Wakili wakiwa katika usikilizwaji shauri la ardhi katika Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya ya Bagamoyo tarehe 31 Agosti 2023. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Na Munir Shemweta, WANMM, BAGAMOYO
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema inaendelea kufanya maboresho makubwa ya kimfumo na muundo kwa lengo la kuewezesaha mambo mengi ya wizara hiyo kufanyika kimfumo,
Hayo yamebainishwa leo tarehe 31 Agosti 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Eng. Anthony Sanga wakati akizindua zoezi la kuondoa mlundikanao wa mashauri katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, uzinduzi uliofanyika wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Amesema, kumekuwa na changamoto kubwa hasa wananchi wa kawaida wanapokwenda ofisi za ardhi kupata namba ya malipo (Control number) hivyo wizara inakuja na mfumo utakaomuwezesha mwananchi kupata namba hiyo ya malipo mwenyewe.
‘’Kumekuwa na changamoto kubwa hasa wananchi wetu wa kawaida wanapokwenda ofisi zetu za ardhi kupata tu control namba inakuwa changamoto, inakuwa kama ni deal sasa tunakuja na mfumo utakaomuwezesha mwananchi kupata control number mwenyewe’’ alisema Eng Sanga
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, hata suala la kufanya search kwa wananchi wanaotaka kununua nyumba au kiwanja nalo anaweza kufanya mwenyewe ambapo kwa sasa analazimika kutoa fedha ili kufanyiwa.
‘’Mnafahamu mtu akitaka kununua nyumba au kiwanja cha mtu katika kufanya upekuzi anaambiwa pia alipe shilingi elfu arobaini au laki moja afanyiwe haraka haraka nayo pia tunaenda kukomesha, mwananchi atafanya upekuzi mwenyewe’’ alisema Eng. Sanga
Aliongeza kwa kusema, kubwa zaidi katika maboresho hayo ni suala la kulipia kodi ya pango la ardhi ambapo kazi yake inakwenda kukamilika hivi karibuni ambapo wananchi wataweza kulipia kupitia simu ya mkononi sambamba na kupata bili kama wanavyopata katika maji.
‘’Utakapokuwa na namba ya NIDA utapata mambo yote, katika wizara yetu ya ardhi wamelizingatia agizo la Mhe. Rais ambapo kwa kutumia kitambulisho cha NIDA mwananchi atapata taarifa zote kuhusina na masuala ya ardhi’’ alisema Eng Sanga.
Akigeukia zoezi la kuondoa mlundikano wa mashauri ya ardhi, amesema zoezi hilo ambalo uzinduzi wake umefanyika pia kwenye wilaya za Musoma, Tarime, Ifakara pamoja na Tabora katika kipindi cha mwezi mmoja jumla ya mashauri 500 yanatarajiwa kusikilizwa na kutolewa maamuzi.
‘’Katika kipindi takriban siku nane toka kuanza kwa zoezi hili wenyeviti wameweza kusikiliza mashauri 243 katika Mabaraza niliyoyataja ambalo zoezi hilo linaendeshwa’’ alisema Eng Sanga.
Kwa upande wake Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya nchini Stela Tullo ameishukuru Wizara ya Ardhi kupitia Mradi wa Uboreshaji Miliki za Ardhi kwa kuyawezesha Mabaraza kuhakikisha yale yanayoelemewa na migogoro angalau yanapata msaada wa wenyeviti kwenda kwenye mabaraza yenye mashauri mengi na kuyakalia vikao maalum kwa lengo la kusikilizwa na kutolewa maamuzi kwa wakati na haki.