Na Mwamvua Mwinyi
Mkoa wa Pwani umeongoza kwa kushika nafasi ya kwanza kwa tathmini ya Saba (7) ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kwa Mwaka 2022/2023.
Taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa – (OR – TAMISEMI) zimeeleza kuwa Mkoa huo umefuatiwa na Lindi katika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikienda kwa mkoa wa Iringa.
Kwa upande wa nafasi za Halmashauri, Mkoa wa Pwani umefanikiwa kuingiza halmashauri za Kibaha Kibaha Mjini na Kibaha Vijijini katika nafasi kumi za mwanzo.
Kibaha Vijijini ikiwa ni ya 10 huku halmashauri zingine za mkoa huo zikiwa zimeshika nafasi juu ya 100 za mwanzo.
Halmashauri hizo na nafasi zao kitaifa ni Kisarawe (17), Rufiji (25), Bagamoyo (26) na Kibiti (54).
Zingine ni Chalinze (59), Mafia (91) na Mkuranga (93).