NA STEPHANO MANGO, MBINGA
UONGOZI wa Umoja wa Jumuiya ya Wanawake w UWT Mkoani Ruvuma umempongeza Mbunge wa Viti Maalum Mkoa huo Mariam Madalu Nyoka kwa kujenga choo chenye matundu sita cha Club ya Manzese Wilaya Mbinga na kutoa vifaa vya usafi jumla ya milioni 10.2
Akizungumza kwenye halfa ya kukabidhi msaada wa choo hicho Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma Eliza Ngongi alisema kuwa Jumuiya hiyo inampongeza sana Mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi zake mara kwa mara
Ngongi alisema kuwa nimezunguka Wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma nikiwa na Mbunge Nyoka nimeona akiahidi na kutekeleza ahadi zake kwa vitendo, jambo ambalo linaonyesha umakini na uweredi katika uwakilishi
“Natoa Shukruni kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Mariam Nyoka kwa kuwa mmoja wa Viongozi ambao michango na misaada yao kwa Jamii inaonyesha wazi Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025” alisema Ngongi
Uongozi umesema kuwa hatua aliyochukua Mbunge Nyoka ni nzuri kwani imethibitisha ni kwa kiwango gani anaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan
Kwa upande wake Mbunge Mariam Madalu Nyoka alisema kuwa ndani ya miezi 3 toka mei hadi Agosti mwaka huu kwa Wilaya ya Mbinga tu ametumia jumla ya fedha milioni 24,573,000. Kwa ajiri ya kutoa misaada mbalimbali
Alisema kuwa pamoja na kukijenga choo hicho na kukikabidhi kwa wajasiliamali ambao wanafanya shughuli zao kwenye soko hilo pia amefanikiwa kununua geti la kituo cha watoto yatima St. Vicent mbinga milion 2
Nyoka alisema kuwa watoto hao pia amefanikiwa kuwapatia mahitaji mbalimbali ikiwemo mablanket 70, mashuka 45, sabuni, mafuta sukari kg.50, sabuni caton 3 baby shoo 5,
Alisema kuwa kwa upande wa Wajasiriamali wajane (Waviu) aliwapatia mtaji wa mahindi wa milioni 2, pia alichangia ujenzi wa Ofisi ya Ccm Wilaya Mbinga Cement mifuko 100 yenye thamani ya 1,700,000,
Katika kuendelea kuwainua Wajasiriamali wadogo sana wenye mitaji chini ya 5000, aliwaongezea mtaji kila mmoja 15,000 idadi yao ni 72 ambapo jumla ya milioni 1,080,000, aliwapatia
Aidha ametoa viti mwendo kwa watu wenye ulemavu 2, mashuka ya Wagonjwa 40, mashine za kupima presha 2, kupima sukari mashine 2, neti za vitanda vya wagonjwa 30 katika Hospitari ya Mbuyula Mbinga na kuwezesha vikundi 7 vya kilimo cha maharage, mahindi na wahoka mikate kila kimoja kilipewa shilingi 500,000 na kufanya jumla ya milioni 3,500,000./=