Na Said Hamdani, LINDI.
ABIRIA 40 waliokuwa wanasafiri na Basi la Kampuni
ya Maning Nice kutoka mkoani Mtwara kwenda Morogoro wamenusulika kiifo kufuatia
gari walilokuwa wakisafiria kuacha barabara na kupinduka.
Kwa mujibu wa mashuhuda na abiria waliokuwa
wanasafiri na basi hilo walisema ajali hiyo,imetokea mtaa wa Likong’o
Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, August 23 majira ya saa 4:30 asubuhi.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizo aliyetembelea eneo la ajali na Hosptali
ya mkoa you,Sokoine, baadhi ya Abiria Armani Nakuwa,Said Ng’ombo na Cosmas
Milanzi wametaja Chanzo cha Ajali ni kujaribu kuipita Lori la kubeba mizigo la
Kampuni ya Dangote
Abiria hao waliokuwa wanasafiri na basi lenye
namba za usajili T 896 DUY kutoka Mtwara kwenda Morogoro walisema wamepata
ajali kufuatia dereva wa basi lao kulipita lori lililokuwa limesimama eneo
lenye kona mlima Likong’o.
Walisema lori hilo lilikuwa limesimama mlimani
baada ya kuharibika,hiyo dereva wao wakati analipita mbele kulikuwa na pikipiki
na magari mengine yakielekea mikoa ya kusini.
“Mbele yetu kulikuwa na Lori la Dangote
limeharibika,wakati analipita tukakutana na Pikipiki na gari nyingine katika
kuzikwepa basi letu likapoteza mwelekeo” walisema abiria hao.
Abiria hao wamemsifu dereva wa basi kuendesha
mwendo ambao haukuwa na kasi na kuweza kupata nusura ya kutopoteza maisha.
Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo Said Chotani na
Mwanaisha Ally wamedai dereva wa pikipiki alikuwa mbishi kulipisha basi hilo la Maning Nice licha
kupigiwa honi mara kadhaa.
Mashuhuda hao walisema kulikuwa na mwendesha
pikipiki hataki kupisha dereva wa basi
alipojaribu kumkwepa ndipo likakosa mwelekeo kutokana na utelezi uliochangiwa
na mvua iliyokuwa ikinyesha.
Pia,wameeleza baadhi ya abiria wamejeruhiwa maeneo ya mikono na miguu
ambapo walipelekwa Hosptali ya Mkoa
Sokoine kwa matibabu.
Kaimu Mganga Mfawidhi Hosptali ya Sokoine Baraka
Mshamu amekiri kupokea majeruhi 16 kati yao wanaume (11) na wanawake watano
akiwemo mtoto mmoja ambaye akumtaja
jinsi yake.
Amesema kati ya abiria hao wawili wameumia mkono
na mguu wa kulia na kupelekwa chumba cha upasuwaji kwa matibabu na waliobaki
wamepata majeraha madogo madogo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Pili Mande
alipotafutwa kupitia simu yake ya mklononi ili kupata kauli yake hakuweza
kupatikana .
Mmoja wa abiria aliyekuwa akisafiri na basi hilo, Said Ng’ombo akielezea jinsi ilivyotokea ajali hiyo. |