Vyumba vipya vya madarasa katika shule ya msingi Songambele, halmashauri ya Nsimbo.
Kulia Mkurugenzi wa halmashauri ya Nsimbo Mohamed Ramadhan akipokea mwenge wa Uhuru kutoka kwa mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda, bi. Sophia Kumbuli.
Na Zillipa Joseph, Katavi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2023 bwana Abdallah Shaib Kaim amezindua vyumba viwili vya madarasa ya shule ya msingi Songambele iliyopo katika halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mapnda mkoani Katavi
Ongezeko la vyumba hivyo vya madarasa unaelezwa kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani na kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunzia.
Akisoma taarifa ya mradi huo kwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Gidas Mwashala alisema mradi huo uliibuliwa na halmashauri mwaka 2020/2021, kuanza kutekelezwa mwezi April 2023 na ulikamilika Juni 2023.
Aliongeza kuwa shule ilipokea kiasi cha shilingi milioni 40 kwa ajili ya kutekeleza mratibu huo na fedha zilizotumika ni shilingi 39,388,800/- fedha ziliizobaki 611,200/-.
Akizindua vyumba hivyo vya madarasa kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa bwana Abdallah Shaib Kaim alisema serikali ya awamu ya sita inaendelea kuboresha mazingira ya shule mbalimbali nchini kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.
Aliongeza kuwa Mwenge wa Uhuru licha ya kuridhika kuuzindua mradi huo lakini umetoa maelekezo ya kufanya marekebisho katika maeneo machache ndani ya siku tatu zijazo.
Awali Mkuu wa wilaya ya Mpanda bi. Jamila Yusuf alisema mwenge wa Uhuru katika halmashauri ya Nsimbo utakimbizwa kilomita 198 na kupitia miradi10 yenye thamani ya SHILINGI 897,052,427/-.