NAIBU Waziri wa Kilimo,Anthony Mavunde,akitoa maelezo katika banda wakati wa kongamano la ujuzi na ajira lililowakutanisha wahitimu wa Programu ya Kukuza Ajira na Ujuzi kwa Maendeleo Afrika (E4D) na waajiri ili kushirikishana katika fursa za soko la ajira lililoandaliwa kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) lililofanyika leo Agosti 24,2023 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Kilimo,Anthony Mavunde,akipata maelezo katika mabanda mbalimbali wakati wa kongamano la ujuzi na ajira lililowakutanisha wahitimu wa Programu ya Kukuza Ajira na Ujuzi kwa Maendeleo Afrika (E4D) na waajiri ili kushirikishana katika fursa za soko la ajira lililoandaliwa kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) lililofanyika leo Agosti 24,2023 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Kilimo,Anthony Mavunde,akizungumza katika kongamano la ujuzi na ajira lililowakutanisha wahitimu wa Programu ya Kukuza Ajira na Ujuzi kwa Maendeleo Afrika (E4D) na waajiri ili kushirikishana katika fursa za soko la ajira lililoandaliwa kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) lililofanyika leo Agosti 24,2023 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA Anthony Kasore ,akizungumza wakati kongamano la ujuzi na ajira lililoandaliwa kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) lililofanyika leo Agosti 24,2023 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula,akizungumza wakati kongamano la ujuzi na ajira lililoandaliwa kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) lililofanyika leo Agosti 24,2023 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Mkuu wa Chuo Cha ufundi Cha Veta Dodoma Stanslaus Ntibara,akizungumza wakati kongamano la ujuzi na ajira lililoandaliwa kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) lililofanyika leo Agosti 24,2023 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo,Anthony Mavunde (hayupo pichani) wakati wa kongamano la ujuzi na ajira lililoandaliwa kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) lililofanyika leo Agosti 24,2023 katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
NAIBU Waziri wa Kilimo,Anthony Mavunde amewaomba waajiri nchini kuendelea kuwekeza kwa kuwatumia vijana wenye ujuzi kwa kuwapatia fursa za kazi na mafunzo ili waweze kuendeleza ujuzi wao na kuchangia katika ukuaji wa biashara zenu.
Naibu Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo leo Agosti 24,2023 jijini Dodoma katika kongamano la ujuzi na ajira lililowakutanisha wahitimu wa Programu ya Kukuza Ajira na Ujuzi kwa Maendeleo Afrika (E4D) na waajiri ili kushirikishana katika fursa za soko la ajira.
” Kumbukeni kuwa kuwekeza kwa vijana wenye ujuzi ni muhimu kwa kuwa nguvu kazi yenye tija na wanachangia katika kujenga jamii imara na taifa lenye maendeleo endelevu,”amesema Mavunde.
Pia Mavunde amehimiza wahitimu wa Mradi wa Ujuzi na Ajira kwa Maendeleo ya Africa (E4D) kuwa na
ujasiri na kujiamini katika kutumia ujuzi wao na kuanzisha miradi yao wenyewe.
Amesema uaminifu, uadilifu na bidii katika kazi ni vigezo muhimu katika mafanikio kwenye ajira ya kuajiriwa au kujiajiri.
Amesema Tanzania ina fursa nyingi za ujasiriamali na mahitaji makubwa katika soko la ajira.
Mavunde amesema kupitia mafunzo hayo vijana wamepata ujuzi unaohitajika katika sekta mbalimbali za viwanda, ujenzi, na teknolojia.
“Hii ni fursa nzuri ya kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kujenga ajira kwa wengine. Hivyo, nendeni mkatumia ujuzi wenu vizuri na mkawe mabalozi wa mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa na Vyuo vya VETA nchini,”amesema Mavunde.
Aidha,Mhe.Mavunde ametoa wito kwa wabia wa Maendeleo, na sekta binafsi kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kwa ajili ya kukuza ujuzi na ajira kwa vijana.
“Tunahitaji kuwekeza katika miundombinu bora ya elimu na mafunzo, kuboresha upatikanaji wa mitaji na mikopo kwa vijana wajasiriamali, na kuweka mazingira rafiki ya biashara,”amesema Mavunde
Pia, waendelee kuhamasisha ushirikiano kati ya vyuo vya ufundi, taasisi za elimu na waajiri ili kuhakikisha kuwa mafunzo yanalingana na mahitaji halisi ya soko la ajira.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), CPA Anthony Kasore amesema kongamano hilo ambalo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Ujuzi na Ajira kwa Maendeleo ya Africa (E4D).
Amesema kongamano hilo linapewa umuhimu mkubwa katika kukuza ujuzi na kuimarisha fursa za ajira kwa vijana na wahitimu wa mafunzo ya ufundi stadi.
Kuhusu mradi huu wa E4D amesema Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imechukua jukumu kubwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa kushirikiana na Ofisi ya Wazri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Shirikisho la Waariji nchini (ATE) pamoja na wadau wa maendeleo.
Amesema Mradi huo una lengo la kuongeza ujuzi wa vijana na kuwapa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko la ajira.
” Tunatambua kuwa ujuzi wa ufundi stadi una jukumu muhimu katika kukuza uchumi na kuwawezesha vijana kujiajiri na kuchangia katika maendeleo ya taifa letu,”amesema Mkurugenzi huyo.
Amesema VETA imechukua hatua madhubuti kuhakikisha vijana wanapata mafunzo bora na yanayolingana na mahitaji halisi ya soko la ajira.
“VETA tunajivunia kuwa sehemu ya utekelezaji wa mradi huu. Hii ni fursa muhimu ya kushirikiana na wadau wa maendeleo kutoka Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Korea ya Kusini (KOICA), Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ), Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Norway (Norad), na Umoja wa Ulaya (EU).
“Ushirikiano huu umeturuhusu kupata rasilimali muhimu, teknolojia, na ujuzi wa kisasa unaosaidia kufanikisha malengo yetu katika mradi huu,”amesema Mkurugenzi huyo.
Amesema VETA inatekeleza mradi huo kupitia vyuo vya Dodoma RVTSC, Manyara RVTSC, Lindi RVTSC na Kipawa ICTC.
Amesema shabaha ni kuwafikia vijana 4,000 katika fani za Mechatronics, uchomeleaji viwandani, pamoja na ufundi bomba majumbani na viwandani.
CPA Kasore amesema tayari vijana 3,258 wamehitimu mafunzo hayo ambapo kwa upande wa chuo cha Chuo cha VETA Dodoma ni kufikia vijana 2200 na hadi sasa kimewafikia vijana 1,806.