Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene,akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene,wakati wa  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul,akizungumza wakati wa  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.Xavier Daudi,akizungumza wakati wa hafla ya   makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mry Makondo ,akizungumza wakati wa  hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Bw. Sylvester Mwakitalu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndombo,akitoa taarifa  fupi kuhusu utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandaoni kwa kushirikiana na Taasisi za Umma wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene,akizungumza wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao(e-GA ) kwa namna inavyotengeneza mifumo inayorahisisha utendaji kazi ndani ya Serikali na Taasisi zake.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma  wakati akizindua mfumo wa kielektroni wa kukusanya , kuchakata na kutunza Kumbukumbu za kesi Jinai utakaoimarisha utendaji kazi uliotengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS)
“Mamlaka ya Serikali Mtandao ni Brain ndani ya Serikali imerahisisha sana utendaji wa kazi serikalini na mfumo huu utasaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti makusanyo ya mapato ya Serikali,”amesema Simbachawene
Simbachawene amesema kupitia mfumo huo mpaka sasa zaidi ya kesi za jinai 17,411 zimeshasajiliwa ambapo kati ya kesi hizo 7,361 zimeshafika mwisho na
kutolewa hukumu huku kesi 10,050 zipo Katika hatua mbalimbali za maaumzi.
“Kiukweli,haya ni mafanikio makubwa katika kuboresha utendaji kazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS),lakini pia ni mfano wa kuigwa na taasisi nyingine za
umma zinazohusika na utoaji wa huduma kwa umma,”amesema Simbachawene
Amesema dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025 na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2021/22 -2025/26), yote inatambua nafasi ya TEHAMA katika kufikia
malengo ya Taifa na hivyo kusisitiza juu ya matumizi sahihi ya TEHAMA katika utekelezaji wa shughuli za Serikali na utoaji wa huduma kwa umma.
Pamoja na mambo mengine, Sera ya Taifa ya TEHAMA ya Mwaka 2016, inasisitiza juu ya Serikali kutumia fursa zitokanazo na TEHAMA pamoja na matumizi sahihi na yenye tija ya Mifumo ya TEHAMA,katika kuboresha utendaji kazi wa Taasisi unaosaidia kutatua changamoto za kiutendaji, kudhibitimakusanyo ya mapato ya Serikali, kujenga na kuboresha uwezo,pamoja na kuimarisha mawasiliano miongoni mwa wadau wa Serikali Mtandao.
“Tumekusanyika hapa kwa lengo la kukabidhi Mfumo wa Kieletroni wa Usimamamizi wa Kesi,ambao unatambulika kama ‘Case Management Information System’(CMIS),pamojanaTovuti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka  liyosanifiwa na kujengwana Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA),kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS)kwa kuzingatia sheria, kanuni, viwango na miongozo iliidhinishwa,”ameeleza Simbachawene

Amesema kuwa lengo kuu la Mfumo wa CMISni kurahisisha utendaji kazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS)katika kushughulikia kesi mbalimbali,usimamizi wa uendeshaji wa kesi za jinai,ambao utaweka uwazi na kupunguza malalamiko kwa wananchi, juu ya maamuzi mbalimbali yanayotolewa na Mahakama.

Aidha, amesema Tovuti ya Taifa ya Mashtaka imejengwa kwa lengo la kusaidia utoaji wa taarifa sahihi kwa wananchi zinazohuasiana na shughuli za Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS).

Hata hivyo amezitaka Taasisi nyingine za umma ambazo bado zina
kiwango kidogo cha utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao kuongeza juhudi
katika matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu yao kama 
Sheria ya Serikali Mtandao ya Mwaka 2019 inavyoelekeza.

”Ni wajibu wenu kuweka jitihada za Makusudi ili kuhakikisha kuwa mnafaidika na fursa zitokanazo na matumizi ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi lakini pia kutimiza azma ya Serikali ya awamu yaSita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa na Serikali na Kidijiti.”amesisitiza

Waziri Simbachawene amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kisera na kisheria yatakayoiwezesha e-GA kuendelea kutekeleza jitihada hizo za Serikali Mtandao kwa ufanisi zaidi.

”Ni jukumu la e-GA kuendelea na tafiti mbalimbali ili kuleta bunifu za
Mifumo ya TEHAMA itakayoliwezesha taifa kufanikiwa kuimarisha sekta
mbalimbaliili kufikia uchumi wa kidijiti.”amesisitiza

Kwa upande wake Naibu Waziri, Wizara ya Katiba na Sheria Mhe.Pauline Gekulu amesema mfumo huo ni muhimu hasa kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza matumizi yake Hali itakayo saidia kuimarisha na kurahisisha utoaji wa haki kwa wananchi.

Amesema katika kupitia dhamira hiyo huduma za serikali zitatolewa kidigitali na kumrahisishia mwananchi kupata huduma kwa haraka zaidi mahali walipo.

“Sote tunafahamu kuwa haki ni Suala muhimu sana na inapaswa kutolewa kwa wakati kwani haki iliyochelewa na sawa na haki iliyonyimwa hivyo Kupitia Mfumo wa TEHAMA tunataka kuhakikisha haki zote zinatolewa kwa wakati, “amesisitiza Mhe.Gekul

Amesema, Sekta ya Sheria imejiwekea malengo thabiti katika kuboresha utendaji kazi wake kwa kutumia mifumo ya TEHAMA kupitia programu ya e-justice kuwezesha kupata taarifa za kesi mbalimbali zilizoshughulikiwa na hatua zilizofikia.

“Mfumo huu umeunganishwa Katika mfumo wa ubadilishanaji taarifa serikalini (GoVESB)na Hadi Sasa tayari unabadilishana taarifa za mifumo ya Jeshi la polisi pamoja na PCCB, “amefafanua.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndombo,amesema malengo madhubuti ya mfumo huo ni kuhakikisha Taasisi zote za Umma zinaenda na wakati kwa kutumia TEHAMA.

” Mfumo huo umejengwa kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa taarifa sahihi zinazohusu uendeshaji wa mashtaka na kusaidia katika uandaaji wa mipango ya ofisi na utoaji maamuzi mbalimbali pamoja na uandaaji wa taarifa zinazowasilishwa kwenye mamlaka nyingine.”amesema Mhandisi Ndombo
Naye Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Sylvester Mwakitalu amesema kupitia Mfumo huo utamsaidia kuharakisha kesi zilizokuwa zinalundikana na kusababisha wananchi kusubiri kwa muda mrefu na kupoteza imani na Serikali.
“Tunaishukuru Mamlaka ya Serikali Mtandao kwa kutengeneza mfumo huu ambao kwa sasa naweza kufuatilia jinsi kesi zote zinavyoshughulikiwa na pale nitakapogundua kuwa kuna jalada limechelewa hapo hapo nauliza sababu za kuchelewa na linashughilikiwa kwa haraka,”amesema Mwakitalu