Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene,akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene,wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pauline Gekul,akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw.Xavier Daudi,akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Bi.Mry Makondo ,akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Bw. Sylvester Mwakitalu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndombo,akitoa taarifa fupi kuhusu utekelezaji wa Sera ya Serikali Mtandaoni kwa kushirikiana na Taasisi za Umma wakati wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene,akizungumza wa hafla ya makabidhiano ya Mfumo wa Kielektroniki wa kukusanya,kuchakata na kutunza kumbukumbu za kesi za Jinai (Case Management Information System ) na Tovuti ya Ofisi ya Mashtaka hafla iliyofanyika leo Agosti 23,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.George Simbachawene ameipongeza Mamlaka ya Serikali Mtandao(e-GA ) kwa namna inavyotengeneza mifumo inayorahisisha utendaji kazi ndani ya Serikali na Taasisi zake.
Amesema kuwa lengo kuu la Mfumo wa CMISni kurahisisha utendaji kazi wa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS)katika kushughulikia kesi mbalimbali,usimamizi wa uendeshaji wa kesi za jinai,ambao utaweka uwazi na kupunguza malalamiko kwa wananchi, juu ya maamuzi mbalimbali yanayotolewa na Mahakama.
Aidha, amesema Tovuti ya Taifa ya Mashtaka imejengwa kwa lengo la kusaidia utoaji wa taarifa sahihi kwa wananchi zinazohuasiana na shughuli za Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS).
Hata hivyo amezitaka Taasisi nyingine za umma ambazo bado zina
kiwango kidogo cha utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao kuongeza juhudi
katika matumizi ya TEHAMA katika utekelezaji wa majukumu yao kama
Sheria ya Serikali Mtandao ya Mwaka 2019 inavyoelekeza.
”Ni wajibu wenu kuweka jitihada za Makusudi ili kuhakikisha kuwa mnafaidika na fursa zitokanazo na matumizi ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi lakini pia kutimiza azma ya Serikali ya awamu yaSita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwa na Serikali na Kidijiti.”amesisitiza
Waziri Simbachawene amesema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kisera na kisheria yatakayoiwezesha e-GA kuendelea kutekeleza jitihada hizo za Serikali Mtandao kwa ufanisi zaidi.
”Ni jukumu la e-GA kuendelea na tafiti mbalimbali ili kuleta bunifu za
Mifumo ya TEHAMA itakayoliwezesha taifa kufanikiwa kuimarisha sekta
mbalimbaliili kufikia uchumi wa kidijiti.”amesisitiza
Kwa upande wake Naibu Waziri, Wizara ya Katiba na Sheria Mhe.Pauline Gekulu amesema mfumo huo ni muhimu hasa kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza matumizi yake Hali itakayo saidia kuimarisha na kurahisisha utoaji wa haki kwa wananchi.
Amesema katika kupitia dhamira hiyo huduma za serikali zitatolewa kidigitali na kumrahisishia mwananchi kupata huduma kwa haraka zaidi mahali walipo.
“Sote tunafahamu kuwa haki ni Suala muhimu sana na inapaswa kutolewa kwa wakati kwani haki iliyochelewa na sawa na haki iliyonyimwa hivyo Kupitia Mfumo wa TEHAMA tunataka kuhakikisha haki zote zinatolewa kwa wakati, “amesisitiza Mhe.Gekul
Amesema, Sekta ya Sheria imejiwekea malengo thabiti katika kuboresha utendaji kazi wake kwa kutumia mifumo ya TEHAMA kupitia programu ya e-justice kuwezesha kupata taarifa za kesi mbalimbali zilizoshughulikiwa na hatua zilizofikia.
“Mfumo huu umeunganishwa Katika mfumo wa ubadilishanaji taarifa serikalini (GoVESB)na Hadi Sasa tayari unabadilishana taarifa za mifumo ya Jeshi la polisi pamoja na PCCB, “amefafanua.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mhandisi Benedict Ndombo,amesema malengo madhubuti ya mfumo huo ni kuhakikisha Taasisi zote za Umma zinaenda na wakati kwa kutumia TEHAMA.