Tanzania imeshiriki katika mkutano wa Mawaziri wa masuala ya wanawake wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola. Mkutano huo wa siku tatu unafanyika tarehe 21 – 23 Agosti 2023 nchini Bahamas. Katika picha ni ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Asha Rose Migiro, Balozi Mstaafu wa Tanzania nchini Uingereza, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Patrick Golwike na Afisa Maendeleo ya Jamii Regina Mollel kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.