Watalii waliyowasili na trni ya Rovos wakipiga picha ya ukumbusho mara baada ya kuwasili katika kituo cha TAZARA jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya watalii wakifurahia kuhitimisha safari yao mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam
Afisa Utalii Mkuu, Alistidia Karaze akizungumza na Meneja wa ROVOS treni wakati wa Mapokezi wa treni hiyo.
Muongoza Watalii wa kampuni ya TAKIMS Holiday akitoa maelekezo kwa Mhudumu wa Treni ya ROVOS.
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki mapokezi ya treni ya kitalii ya Kampuni ya ROVOS iliyowasili nchini Tanzania leo ikiwa na watalii 31 wakitokea nchini Angola. Treni hii kawaida hufanya safari zake kuanzia nchini Afrika ya Kusini mpaka Tanzania. Kwa mwaka huu ni safari ya tatu kwa treni hiyo kuleta watalii nchini.
Watalii hao wameonyesha kuvutiwa na mandhali ya maeneo ya Tanzania waliyopita wakati wa kuelekea jijini Dar es Salaam. Wakiwa nchini watembelea Visiwa vya Zanzibar, Bagamoyo, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Hifadhi ya Nyerere. Filamu ya Tanzania the Royal Tour iliyoasisiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuleta matokeo Chanya na kuvutia watalii kutoka mataifa mbalimbali kuja kutembelea vivutio vya utalii vya Tanzania.
Hayo yamesemwa na Afisa Utalii Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania, Alistidia Karaze wakati wa mapokezi ya watalii hao katika kituo cha treni ya TAZARA jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa kundi hiili limejumuisha watalii kutoka nchi za Ujerumani, Uingereza, Marekani na Dernmark.
Kwa upande Meneja wa Treni, Bw. Lyle Ontong amesema safari hii imechukuwa siku 65 ambapo ilianzia Afrika kusini kuja Tanzania, ikaenda nchini Angola na kurudi Tanzania ambapo inatarajia kuondoka Agosti 21, 2023 kurudi Afrika kusini ikiwa na Watalii 67kutokaa Ujerumani ambao wataanzia safari yao katika kituo cha TAZARA jijini Dar es Salaam.
Watalii waliyowasili na treni ya Rovos wameonyesha kuvutiwa na wamefurahishwa na muonekano wa maeneo waliyopita jijini Dar Es Salaam na kulinganyisha na baadhi ya maeneo ya nchi nyingine walizopita na kushauri kuwa, Watanzania tunapaswa kutunza vivutio vyetu vya asili pomoja na mazingira ya miji kwa faida ya vizazi vya baadaye na pia kuwavutia watalii wengi zaidi.