Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu, Prof. Jamal Katundu akifafanua lengo la serikali ya awamu ya Sita la kukifanya chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu Yombo Dar es salaam, kuwa cha kisasa na chenye kukidhi mahitaji yote muhimu kwa Watu wenye Ulemavu.
Sehemu ya wanafunzi katika Chuo cha Ufundi Stadi na MarekebishoYombo wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Jamal Katundu (hayupo pichani).
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu, Prof. Jamal Katundu, na Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA, Mark Bryan Schreiner ( wa pili kushoto) na Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Uswisi, Holger Tausch (wa pili kulia), wakiwa na watumishi wa Ofisi hiyo na UNFPA mara baada ya uzinduzi wa jengo la wagonjwa wanaosubiri tiba katika zahanati ya chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu Yombo Dara es salaam
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu, Prof. Jamal Katundu (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA, Mark Bryan Schreiner (katikati) na Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Uswisi, Holger Tausch, wakipanda mti wa kumbukumbu ya uzinduzi wa jengo la wagonjwa wanaosubiri tiba katika zahanati ya chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu Yombo Dara es salaam
Na Mwandishi Wetu: Dar es Salaam
SERIKALI kwa kushirikiana na wadau likiwemo Shirika la UNFPA na Ubalozi wa Uswisi nchini wanajipanga kufanya tathmini ya mahitaji ya Chuo cha Ufundi na Marekebisho kwa watu wenye Ulemavu Yombo Dar es Salaam ili ku kifanya kuwa chuo bora na cha kisasa.
Amesema lengo la serikali ya awamu ya Sita ni kukifanya chuo hicho kuwa cha kisasa na chenye kukidhi mahitaji yote muhimu kwa watu wenye ulemavu.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu, Prof. Jamal Katundu wakati akizindua jengo la wagonjwa wanaosubiri tiba katika zahanati ya chuo hicho leo tarehe 18 Agosti 2023.
Profesa Katundu amesema Shirika la UNFPA na Ubalozi wa Uswisi wamefanikisha ujenzi wa jengo hilo pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya zahanati kwa gharama ya Dola za Marekani 40,000 sawa na Shilingi milioni 92.
Mkurugenzi Mkazi wa UNFPA, Mark Bryan Schreiner amesema moja ya malengo ya shirika hilo ni kusaidia vijana wakiwemo wenye ulemavu katika masuala ya kuwajengea uwezo ukiwemo wa kielimu.
Mkuu wa Ushirikiano wa Ubalozi wa Uswisi, Holger Tausch amesema mwaka 2013 Serikali ya Uswisi iliisaidia UNFPA kuanzisha programu ya kuwalinda vijana (SYP) katika nchi za Afrika ambapo mwaka 2021 programu hiyo pia ilianzishwa Tanzania, Rwanda na Msumbiji.
Kaimu Mkuu wa chuo hicho, Mariam Chellangwa amesema chuo hicho kilianzishwa mwaka 1973 na kwa sasa kina jumla ya wanafunzi wenye ulemavu 104 na kubainisha ujenzi wa jengo hilo utaimarisha huduma za Afya za wanafunzi hao na jamii inayo wazunguka.