WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji,akizungumza wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara wa jijini la Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali kilichofanyika jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe,,akizungumza wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara wa jijini la Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali kilichofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa Kikao kazi cha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji,na wafanyabiashara wa jijini la Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali kilichofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji,(hayupo pichani) akizungumza wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara wa jijini la Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali kilichofanyika jijini Dodoma.
Wafanyabiashara mbalimbali wakichangia hoja wakati wa Kikao kazi na wafanyabiashara wa jijini la Dodoma,wajasiriamali na wafanyabiashara pamoja na majukwaa yanayojihusisha na ujasiriamali na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji.
Na.Alex Sonna-DODOMA
Serikali imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara kwa kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wawekezaji na wafanyabiashara nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji alipokutana wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kutatua changamoto zinawazowakabili.
Dk. Kijaji amesema kuwa tangu kuanza kutekelezwa kwa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara hapa nchini (Blue Print), Serikali imefanikiwa kuondoa kodi, tozo na ushuru mbalimbali 374 kati ya 380.
“Tulianza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara mwaka 2019 na tulitamani kuondoa kodi, tozo pamoja na ushuru mbalimbali zilizokuwa zikilalamikiwa na wafanyabiashara nchini ambazo zilikuwa 380 kwa miaka Mitano.
Lakini leo tuko mwaka wa Nne tunatekeleza na tumeshaondoa kodi, tozo na ushuru 374 zimebaki Sita tuu na Serikali ya Awamu ya Sita imedhamiria kuzimaliza changamoto hizi zote lengo likiwa ni kuhakikisha mnafanya biashara katika mazingira mazuri na wawekezaji wanawekeza katika mazingira mazuri na yanayoibuka tunayabeba na kuendelea kushughulika nayo,” amesema Waziri Kijaji.
Dk. Kijaji pia ameagiza kitabu kinachoainisha kodi hizo zilizoondolewa kichapishwe ndani ya wiki moja na kifikishwe kwa Wakuu wa Mikoa ili wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wajue kodi zipi zilizoondolewa kupunguza migogoro kati ya wafanyabishara na serikali.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amempongeza Waziri Kijaji kwa kukutana na kuzungumza na wafanyabiashara hao pamoja na kutatua changamoto na kero zilizokuwa kikwazo katika utekelezaji wa biashara zao.
”Mkoa wa Dodoma upo tayari kupokea wawekezaji na kuongeza idadi ya viwanda ili kuongeza na kukuza mapato ya Serikali na uchumi wa nchi ya Tanzania.”amesema Mhe.Senyamule