Na Mwandishi Wetu, Angola
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, (SADC Panel of Elders) akiwa pamoja na Viongozi wanaounda Kamati ya Utatu ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC- TROIKA) wakijiandaa na Mkutano wa Kamati hiyo unaofanyika leo tarehe 16 Agosti, 2023, Luanda, Angola.
Viongozi hao ni pamoja na Mhe. Hage Geingob, Rais wa Namibia ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa SADC TROIKA, Mhe. Haikande Hichilema wa Zambia ambaye anatarajiwa kuchukua Uenyekiti wa Kamati hiyo na Mhe. Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye ni Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Kamati hiyo ya SADC TROIKA. Pichani pia ni Mhe. Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Lesotho (wa pili kutoka kulia) na Katibu Mtendaji wa SADC, Mhe. Elias Magosi (wa kwanza kushoto).
Rais Mstaafu Kikwete amewasilisha katika Kamati hiyo ya SADC TROIKA Ripoti ya Kamati ya Uangalizi (Oversight Committee) anayoiongoza katika kufuatilia hatua za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kiasiasa ulipo katika Ufalme wa Lesotho.