Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na vijana pamoja na Uongozi wa Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (KATC), wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kutoka kulia) akimsikiliza mnufaika wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), Andrew Kessy wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo kwenye kituo atamizi cha vijana kilichopo Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (KATC), Mkoani Kilimanjaro. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kisare Makori.
Baadhi ya vijana wanufaika Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) wakifuatilia kwa makini maelezo ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani), wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo kwenye kituo atamizi cha vijana kilichopo Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (KATC), tarehe 12 Agosti, 2023, Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akimsikiliza mnufaika wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), Mwanahawa Shehoza (kulia) kuhusu manufaa ya Bustani Jamii alipotembelea chuo hicho kwa lengo la kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, Mkoani Kilimanjaro. Watatu kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kisare Makori.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kisare Makori (kushoto) akieleza jambo wakati wa wakati wa ziara ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) kwenye kituo atamizi cha vijana kilichopo Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (KATC), tarehe 12 Agosti, 2023, Mkoani Kilimanjaro.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (KATC), Witnesss Bashaka (kushoto) akitoa taarifa kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi wakati akikagua maendeleo ya utekelezaji wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) kwenye kituo atamizi cha vijana kilichopo chuoni hapo, Mkoani Kilimanjaro.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (katikati) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kisare Makori (kushoto) wakati wakikagua mashamba darasa katika chou hicho. Kulia ni Katibu wa UVCCM Moshi Vijijini, Bw. Melkiud Pantaleo na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (KATC), Witnesss Bashaka.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Na: Mwandishi Wetu – Kilimanjaro
SERIKALI imeendelea kuwashirikisha vijana katika mipango na programu za kiuchumi ili wajiajiri na kuajiri wenzao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi ameyasema hayo alipokuwa akikagua maendeleo ya utekelezaji wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT) kwenye kituo atamizi cha vijana kilichopo Chuo cha Mafunzo ya Kilimo (KATC), mkoani Kilimanjaro.
Mhe. Katambi amesema serikali imewajengea mifumo mizuri vijana inayowasaidia kupata mitaji ya kuanzisha shughuli za kiuchumi na kuwaasa wanufaika wa BBT kuwa mabalozi wa kilimo biashara nchini ili kukuza uchumi na maendeleo ya nchi Taifa.
Aidha, amesema kuwa utekelezaji wa mradi wa BBT ni dhamira ya serikali chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha vijana wanapata fursa katika sekta za kiuchumi ikiwamo madini, kilimo, mifugo na uvuvi.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Mhe. Kisare Makori amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika mradi huo ili waweze kujikwamua kiuchumi, huku Mnufaika wa BBT, Bw. Orest Kibiki wakimshukuru Rais Samia kwa kutoa kipaumbele kwenye masuala ya vijana.