WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ,akizungumza kwenye Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenyeulemavu, Profesa Joyce Ndalichako,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule.akitoa salamu za Mkoa wake wakati wa Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA Hosea Kashimba,akitoa taarifa ya Mfuko huo wakati wa Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
Rais wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Bw.Tumaini Nyamhokya,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Mhe.Fatma Touqi,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini PSSSF Mhandisi Musa Iyombe,akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa (hayupo pichani), akizungumza kwenye Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua huduma tatu za kidigitali ambazo ni utaratibu wa wanachama wapya kujiunga kwenye Mfuko, mfumo wa kidigitali wa kuanzisha madai ya mafao, uhakiki wa Wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye Ofisi za Mfuko. Uzinduzi huo
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa,akizindua huduma tatu za kidigitali ambazo ni utaratibu wa wanachama wapya kujiunga kwenye Mfuko, mfumo wa kidigitali wa kuanzisha madai ya mafao, uhakiki wa Wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye Ofisi za Mfuko hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, akimwangalia Mstaafu Grace Solomon, wakati akitumia mfumo wa kidigitali wa uhakiki wa Wastaafu kupitia simu janja popote walipo bila kufika kwenye Ofisi za Mfuko, huduma hizo zimezinduliwa leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha Maadhimisho ya Miaka Mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa,amewaagiza waajiri wakamilishe kulipa malimbikizo ya michango ya watumishi na tozo katika mifuko ya hifadhi ya jamii ifikapo Septemba 30 mwaka huu.
Mhe.Majaliwa ametia maagizo hayo leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) zoezi lililoenda sambamba na uzinduzi wa mfumo wa TEHAMA wa Mfuko huo hafla iliyofanyika leo Agosti 12,2023 jijini Dodoma.
“Mifuko yote ya hifadhi ya jamii, lipeni mafao kwa wakati kama mnavyofanya sasa ili kuleta utulivu kwa wanachama. Wazee wastaafu wasisumbuliwe, kumbukeni kuwa sisi sote ni wastaafu watarajiwa,” amesema Mhe.Majaliwa
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ameziagiza taasisi za Serikali kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alilolitoa wakati uzinduzi wa mkongo wa mawasiliano wa 2Afrika na matumizi ya teknolojia ya 5G la kutaka taasisi zote za Serikali ziwe zinasomana ili kurahisisha na kuboresha utoaji wa huduma kwa Watanzania.
Waziri Mkuu amesema kiwango cha thamani ya uwekezaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) imeongezeka hadi kufikia shilingi trilioni 7.98 kwa mwaka 2022/2023 kutoka shilingi trilioni 7.5 kwa hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Juni, 2022.
“Thamani hii ipo katika soko la hisa ambalo ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa mitaji nchini ambapo mfuko huo ni muwekezaji mkubwa wa ndani mwenye hisa katika makampuni makubwa kama CRDB Bank Plc, NMB Bank Plc, Tanzania Breweries Limited, na Vodacom Tanzania Plc. ”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameitaka Mifuko ya Hifadhi ya jamii kufanya uwekezaji wenye tija kwa wanachama na jamii inayolingana na thamani ya fedha za wanachama “Fanyeni utafiti wa kina kubaini masoko ili uwekezaji unaofanywa usilete hasara kwa mifuko. ” amesema
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira,Vijana na Wenyeulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, amesema dhamira ya Rais Dk. Samia ni kuhakikisha mifuko ya hifadhi ya jamii inaendelea kutimiza wajibu wake kwa ufanisi.
Aidha amefafanua A kuwa katika kutekeleza dhamira hiyo kwa vitendo, Rais Dk. Samia alichukua hatua ya kuimarisha mifuko hiyo kwa kutoa sh. trilioni 2.17 kupitia mfumo wa hati fungani kulipa deni la sh. trilioni 4.6 ambalo tangu mwaka 1999 halikuwahi kulipwa.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) CPA Hosea Kashimba,amesema kuwa mfuko huo umefanikiwa kulipa madai ya sh. trilioni 1.03 yaliyorithiwa kutoka katika mifuko iliyounganishwa kwa wanachama na wategemezi 10,273 waliokuwa katika foleni ya muda mrefu.
Hata hivyo amesema kwa kipindi cha miaka mitano hadi kufikia Juni mwaka huu, mfuko huo umelipa sh. trilioni 8.8 kwa wanufaika 262,095, umeweza kulinda na kuongeza thamani ya uwekezaji kutoka sh. trilioni 6.4 hadi sh. trillion 7.9 Juni mwaka huu ambayo ni wastani wa ongezeko la asimilia nne kwa kila mwaka.
“Mfuko unapata mapato yatokanayo na uwekezaji ya wastani wa asilimia nane kwa mwaka, mfuko umeweza kulinda na kuongeza thamani ya mfuko kwa asilimia 27.76 kutoka sh. trilioni 5.83 Julai 2018 hadi sh. trilioni 8.07 Juni mwaka huu,” ameeleza