WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akikata utepe wakati akikabidhi magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu hafla iliyofanyika leo Agosti 7,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akizungumza leo Agosti 7,2023 jijini Dodoma wakati akikabidhi magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu.
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu.
RAIS wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Bw. Tumaini Nyamuhokya ,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani) akizungumza wakati akikabidhi magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akikata utepe wakati akikabidhi magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu hafla iliyofanyika leo Agosti 7,2023 jijini Dodoma.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akiwasha gari mara baada ya kukabidhi magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu hafla iliyofanyika leo Agosti 7,2023 jijini Dodoma.
SEHEMU ya Magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) vilivyokabidhiwa leo Agosti 7,2023 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi,akitoa neno la shukrani mara baada ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,kukabidhi Magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,ameuagiza Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuhakikisha ifikapo Agosti 30 mwaka huu magari yote mabovu ya serikali yaliyoegeshwa kwa muda mrefu katika karakana za wakala huo yatengenezwe na taarifa ya matengenezo hayo apatiwe.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa maagizo hayo leo Agosti 7,2023 jijini Dodoma wakati akikabidhi magari 30 na vifaa vya ofisi za mikoa za Idara ya Kazi na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa wakati wa Sherehe za Sikukuu ya Wafanyakazi (Meimosi), iliyofanyika mkoani Morogoro, Mei mwaka huu.
Aidha amewataka kuongeza weledi katika utendajikazi wake kwa kuzingatia mpango maalum wa matengenezo wa magari ya umma.
”TEMESA,hadi Agosti 30 mwaka huu Mnapaswa kutengeneza magari yote ya serikali yaliyoegeshwa katika karakana zenu kwa muda mrefu kisha taarifa hiyo nikabidhiwe pia nataka muongeza weledi katika utendaji kazi wenu kwa kuzingatia mpango maalum wa matengenezo wa magari ya umma.”amesema Waziri Mkuu
Aidha, aamesema kwa magari ambayo yametumika muda mrefu na matengenezo yake yanatumia gharama kubwa, uwekwe mpango maalum wa kuwakopesha watumishi wa umma kwa kuzingatia sheria, badala ya kuendelea kuegeshwa katika ofisi za halmashauri au karakana za TEMESA.
“Kila idara inapaswa kusimamia matumizi ya magari na kuyatunza ili yaweze kudumu kwa muda mrefu. Magari ya serikali yanapaswa kutumika kwa shughuli za umma, sio binafsi na wapewe madereva wenye uweledi,” amefafanua
katika magari hayo ambayo OSHA imekabidhiwa magari 13, anatarajia wakala huo utaongeza kaguzi katika maeneo ya kazi ili kuendelea kusimamia mazingira bora ya wafanyakazi katika maeneo yao ya kazi.
Pia, kwa Ofisi za Mikoa Idara ya Kazi ambazo zimepatiwa magari 17, ametoa wito kwamba yatumike kwa shughuli za kulinda haki na kuimarisha ushirikiano baina ya mfanyakazi, mwajiri, vyama vya wafanyakazi.
Amesema magari na vifaa hivyo vimetolewa ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais Dk. Samia ambaye aliridhia kutoa fedha za ndani kununua vitendeakazi hivyo, baada ya Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUTCA) Tuamaini Nyamhoka, kueleza kwamba baadhi ya taasisi za serikali zinazoshughulika na masuala ya wafanyakazi zina vitendea kazi vichache.
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amewaagiza Maofisa Masuuli na wanaosimamia usalama kuwafuatilia na kuwachukulia hatua madereva wa serikali wanaoiba mafuta kwenye magari kwani vitendo hivyo ni sawa na uhujumu uchumi wa nchi.
“Natoa maagizo kwa madereva wote wa serikali wazingatie sheria za nchi ikiwemo usalama barabarani. Kuendesha magari ya serikali sio kigezo cha kuvunja sheria. Pia, maofisa masuuli na maofisa usalama fuatilieni kisha mchukue hatua kwa madereva wa serikali wanaodanganya umbali wa safari na kuiba mafuta,” amesema
Waziri Mkuu amesema kuwa wizi wa mafuta katika magari ya serikali ni sawa na vitendo vya uhujumu uchumi, hivyo madereva watakaobaini kufanya vitendo hivyo wachukuliwe hatua.
Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako, amesema ofisi yake itahakikisha inasimamia magari na vifaa hivyo ili vilete tija
”Vitendea kazi hivyo ni muhimu kwani Serikali ya Rais Dk. Samia imedhamiria kwa kutekeleza mikakati ya kuimarisha uwekezaji na kuboresha mazingira ya wafanyakazi.”amesema Prof.Ndalichako
Pia, amesema serikali inaendelea kuimarisha nguvu kazi kupitia programu ya kitaifa ya kukuza ujuzi inayotolewa kwa watumishi wa umma na sekta binafsi.
Kwa upande wake, Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Bw. Tumaini Nyamuhokya amesema kuwa anamshukuru Rais Dkt. Samia kwa kutekeleza maombi yao kwa haraka.
“Wakati wa sherehe za Mei Mosi, 2023 tuliiomba Serikali ikumbuke taasisi zake za mikoani. Tulimuomba Mheshimiwa Rais kwa sababu tunaona hali halisi huku mikoani. Hatukutegemea kama utekelezaji ungekuwa wa haraka hivi, tunamshukuru sana. Tunatumaini hayo magari yataongeza ajira kwa madereva 30.”
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri (ATE), Meneja wa Kanda ya Kati Dodoma, Bw. Selestine Leonard amewataka waajiri na wafanyakazi waendelee kuzingatia usalama wa mahali pa kazi.
“Niwasihi waendelee kuzingatia uadilifu na hasa kujali muda wa kazi. Pia wajiepushe na vitendo vya rushwa mahali pa kazi. Sisi ATE tutaendelea kushirikiana nao,” amesema