Mkaguzi wa Vyombo vya Usafiri wa Majini TASAC, Kapten Philbert Katili kutoka Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) akizungumza katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya namna kazi ya ukaguzi inavyofanyika wakati akitoa elimu katika maonesho hayo.
NA JOHN BUKUKU, MBEYA
Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) limewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri wa majini kuzingatia sheria na kanuni ili usafiri huo uendelee kuleta tija katika kusafirisha abiria pamoja na mizigo.
Akizungumza katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane kwenye Viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya, Mkaguzi wa Vyombo vya Usafiri wa Majini TASAC, Kapten Philbert Katili, amesema kuwa wanaendelea kusimamia usalama wa vyombo vya majini pamoja na hakikisha kunakuwa na vyombo uokoaji.
Kapten Katili amesema kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa sekta ya kilimo wameshiriki maonesho ya nanenane kwa ajili ya kuwafikia watu wengi ilia kutoa elimu.
“Wakulima wanatumia usafiri wa majini katika kusafirisha mazao yao kwenda maeneo mbalimbali kutafuta masoko hivyo ni muhimu wakawa na uwelewa katika usafiri wa majini” amesema Kapten Katili.
Amesema kuwa elimu ya usalama wa usafirishaji wa mizigo kwa njia ya maji ni muhimu kwa wakulima ili waweze kuendelea kutumia bila kuwa na wasiwasi.
“TASAC tunaendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia maonesho mbalimbali kutokana na elimu ya usalama wa vyombo vya majini tunayoitoa ni muhimu kwa wananchi kuelewa katika kuongeza usalama” amesema Kapten Katili.
Amesema TASAC inaendelea kusimamia sheria na taratibu zilizopo ili kuhakikisha usalam wa vyomvo vya majini unakuwa ni wa wakati wote na ni muhimu wamiliki na watumiaji wa vyombo hivyo kuzingatia sheria na kanuni zake ili kuhakikisha vyombo hivi vinafanya safari majini kwa usalama.