Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akizungumza na vijana pamoja na wadau wa asasi za kiraia zinazojishughulisha na masuala ya vijana katika kongamano la vijana lililofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya vijana wakifuatilia kwa makini hotuba ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kongamano la vijana lililofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi na Wadau wa Asasi za Kiraia zinazojishughulisha na masuala ya vijana katika kongamano la vijana wakifuatilia mada mbalimbali katika kongamano hilo.
Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Leonard Mchau akieleza jambo wakati wa kongamano hilo la vijana lililofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwiga Mbesi akifafanua jambo wakati wa kongamano hilo la vijana lililofanyika jijini Dodoma
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Vijana mkoani Dodoma (DOYODO), Rajab Juma akieleza jambo wakati wa kongamano hilo la vijana lililofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya wawezeshaji wakitoa mada katika kongamano hilo la vijana (Tanzania Youth Forum) lililofanyika jijini Dodoma.
Mwakilishi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Tumsifu Mwasamale akitoa salamu wakati wa kongamano la vijana lililofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya Viongozi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia mada mbalimbali katika kongamano hilo la vijana (Tanzania Youth Forum) lililofanyika jijini Dodoma.
PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)
Na: Mwandishi Wetu – Dodoma
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi amesema serikali inaandaa Mfumo wa Taifa wa uratibu na tathmini wa afua za masuala ya maendeleo ya vijana nchini utakaosaidia kuwatambua na kuwaratibu wadau.
Kutokana na hilo, amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo na Msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali kuzifanyia tathmini asasi za kiraia zinazoshughulikia masuala ya vijana ili kujua utendaji kazi wake na kama zinakidhi tija vijana.
Mhe. Katambi ameyasema hayo Agosti 3, 2023 kwenye uzinduzi wa kongamano la vijana lililoandaliwa na asasi za kiraia 32 zinazojishughulisha na masuala ya vijana.
“Niwaagize Katibu Mkuu na Msajili wa mashirika mfanye tathmini ili kuhakikisha asasi hizi zinatekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na malengo ya serikali ili kuleta tija kwa vijana nchini,”amesema.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya Vijana mkoani Dodoma (DOYODO), Rajab Juma ameomba serikali kuzitengea ruzuku asasi zinazojihusisha na masuala ya vijana kama ilivyo kwa vyama vya siasa ili kuwafikia kundi kubwa la vijana katika kujenga kesho yao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Idara ya Demokrasia, Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bret Saalwaechter ameipongeza serikali ya Tanzania kwa ushirikishwaji wa vijana, wanawake na Watu wenye Ulemavu katika kuwaletea maendeleo na kushughulikia changamoto zao.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Freedom House, Daniel Lema, amesema bado kuna kundi la vijana wanashindwa kutumia fursa zinazowazunguka ili kutengeneza kipato na kuishia kulalamika.
Kongamano hilo lomeongozwa na Kauli mbiu isemayo “Ushiriki wa Vijana kwenye Uongozi na Utawala Bora kwa Maendeleo ya kiuchumi”