Mbunge wa jimbo la urambo mkoani Tabora Margaret Sita akipokea taulo za kike zilizotolewa kwa ajili ya wanafunzi wa shule za Sekondari na msingi kutoka kwa Meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya magharibi Christopher Migoha aliyevaa miwani akiwa na baadhi ya madiwani aliyevaa nguo ya mistari ya mpunda milia ni Diwani wa kata ya kapilula ,Paulo Shija na Diwani wa kata ya kiyungi ,Ahmed Seif na mtumishi wa mamlaka wa TMDA.
Madiwani wa viti maalum wa wilaya ya Urambo wakishuhudia mbunge wa jimbo hilo akipokea Taulo za kike zilizitolewa kwa ajili ya wanafunzi wilayani humo.
Meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya magharibi Christopher Migoha akiwaonesha madiwani viti maalum wa halmashauri ya wilaya ya Urambo Paketi ya Taulo za kike zilizotolewa kwa ajili ya wanafunzi wilayani humo.
Na Lucas Raphael,Tabora
Mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA Mkoani Tabora wametoa taulo za kike pateki (1000) kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari wanaokutana na changamoto wawapo shuleni
makabidhiano hayo ya yamefanyika katika ofisi ya mbunge wa jimbo la urambo mkoani hapa Margaret Sita ambaye alisema kumekuwa na uhitaji mkubwa wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za Sekondari na msingi .
Alisema kwamba taulo hizo zitaenda kuwanufaisha wanafunzi wa shule mbalimbali kama itakavyoratibiwa kwa kuangalia vigezo vya shule zenye uhitaji zaidi
“Tumekuwa na uhitaji wa taulo za kike japokuwa tumeendelea kupambana na changamoto hiyo kwa kuleta taulo za kike mara kwa mara na wakati mwingine tunawafundisha wanafunzi kujitengenezea taulo za kienyeji ambazo nazo huwafaa lakini kwa ujio wenu TMDA kumeleta tija kubwa kwetu” Alisema Margaret Sita
kwa upande wake kaimu afisa elimu wa shule za Sekondari wilayani urambo Rudia Masatu alikili changamoto zinazowakuta wanafunzi wa jinsi ya kike ambao wengi wao hulazimika kusitisha baadhi ya vipindi darasani wanapoingia kwenye siku zao hivyo ameshukuru na kumpongeza mbunge kwa kuwaleta wageni hao.
Meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya magharibi Christopher Migoha aliwataka madiwani kuiga mfano huo kwa kuwawezesha wanafunzi waliopo kwenye shule za Sekondari zilizopo kwenye kata zao ili kuwasaidia katika changamoto ya kukatisha masomo yao.
“Madiwani mliopo hapa jifunzeni kitu kutoka kwetu angalieni uhitaji uliopo kwenye kata zenu pia wawezesheni watoto wa jinsi ya kike wao wanakabiliwa na changamoto kubwa kwa hiyo jitahidini kuwapa taulo za kike” alisema Christopher Migoha
Naye katibu wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya urambo Himid Tweve na madiwani wa kata za kapilula Paulo Shija na kiyungi Ahmed Seif walishiriki makabidhiano hayo wakisema agizo la walilopewa wataenda kulitekeleza.