Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Tanzania Commercial Bank (TCB) mkoani Geita lililopo eneo la soko la dhahabu ikiwa ni moja na mipango na mikakati ya Benki hiyo kusogeza huduma za kifedha kwa wananchi na wafanya biashara wa eneo hilo. kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Sabasaba Moshingi pamoja na Meneja wa Benki wa Tawi hilo Andrew Mziray. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika hivi karibuni
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigella (kilia), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania commercial Bank Sabasaba Moshingi wakifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya Biashara Tanzania (TCB) mkoani Geita lililopo eneo la soko la dhahabu ikiwa ni moja na mipango na mikakati ya Benki hiyo kusogeza huduma za kifedha kwa wananchi na wafanya biashara wa eneo hilo. Hafla ya uzinduzi huo imefanyika hivi karibuni
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela leo amefungua tawi jipys la Tanzania Commercial Bank(TCB) Mkoani humo ikiwa ni katika harakati za kupanua wigo wa biashara na kufungua fursa mbalimbali katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tawi hilo Shigela alisema kuwa kufunguliwa kwa tawi hilo Kutawezesha kupatikana kwa ajira za kudumu kwani takribani watumishi 800 wameajiriwa katika tawi hilo.
Shigela aliongeza kuwa benki hiyo itawezesha wafanyabiashara wadogo wakati na wale wakubwa na vikundi vidogovidogo kuendelea kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wafanyabiashara hao kuendelea kukuza mitaji yao.
“Sisi wana Geita tutafaidika na mikopo hii, na riba yake ni miongoni mwa benki inayotoa riba nzuri kuliko benki zingine, utapewa riba nzuri na muda wa kutosha kuzalisha fedha zako na kuirudisha”Alisema Shigela.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi alisema kuwa kwa kipindi cha miaka 10 bank imeuza mali za bank kutoka bilioni 121 hadi kufikia trillion 1 na bilioni 400 na kuongeza idadi ya matawi kutoka 30 hadi kufikia matawi 80 hivyo kuongeza ajira kutoka wafanyakazi 400 hadi kufikia wafanyakazi 1200.
Kwa upande wake meneja wa Tanzania Commercial Bank TCB Andrew Mzirai alisema kuwa Benki hiyo imejipanga kutoa fursa kwa wachimbaji wadogowadogo kwa kuwapa mikopo kwa ajili ya vifaa vya kufanyia shughuli za uchimbaiji.