Na Lucas Raphael,Tabora
Mahakama ya kuu Kanda ya Tabora ,Imesema itatoa hukumu ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Elick Komanya Kitwala septemba 15 mwaka huu baada ya kukata rufaa ya kupiga maamuzi yote yaliyotolewa na mahakama ya wilaya ya Tabora .
Mahakama ya wilaya katika umuazi wake kwenye shauri la madai ya fidia ya shilingi milioni 140 dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Elick Komanya Kitwala na kuamuru amlipe mdai Shilingi milion 80 kutokana na vitendo vya udhalilishaji.
Akitoa uamuzi huo jana Jaji Dkt Mwajuma Kadilu wa mahakama kuu kanda ya Tabora alisema kwamba baada ya kusikiliza mawakili wa pande zote mbili mahakama hiyo itaoa hukumu wa Kesi hiyo septemba 15 mwaka huu .
Alisema makahama kuu itatoa hukumu hiyo siku ya Ijumaa ambayo itakuwa Tarehe 15.9.2023 na mawakili wote watatu walikubaliana na uamuzi wa Jaji .
Upande wa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Tabora ,Elick Komanya Kitwala aliwakilishwa na wakili wa Kujitegemea wawili ambao ni Issa Mavura na Jeremia Mtobesya ambao waliomba mahakama kuu kutupilia mbali hukumu iliyotelewa Disemba 30 mwaka jana na hakimu Jovith Kato wa makahakama ya mkoa wa Tabora.
Upande wa Alex Ntonge aliwakilishwa na wakili Kelvin Kayaga .ambaye alikubaliana na hukumu ilitolewa na mahakama ya hakimu wa mkoa wa Tabora kwani ilifuata taratibu zote za kimahakama .
Wakili Kelvin aliomba mahakama hiyo kutupilia mbali rufaa hiyo kwani haikufuata taratibu za kisheria.
Hadi Hukumu hiyo ilitolewa siku ya Dideemba 30 mwaka jana na hakimu Jovith Kato huyo alikuwa ni Hakimu wa Tatu kusikiliza shauri hilo ambalo awali lilianza kusikilizwa na hakimu Sigwa Nzige lakini mdaiwa alimkataa ndipo likaamishiwa kwa hakimu mkazi mfawidhi wa Wilaya ya Tabora Demotrio Nyakunga ambaye pia hakuendelea nalo.
Komanya ambaye alienguliwa katika nafasi ya ukuu wa Wilaya na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Juni 19/2021 ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya Madai fidia ya Shilingi milioni 140 kutokana na vitendo vya udhalilishaji alivyomfanyia Alex Ntonge Januari 05/2021.
Katika shauri hili la Madai namba 04/2021 mdai alitaka alipwe nafuu ya shilingi milioni 80 kutokana na kuzuiwa uhuru wake, Milioni 30 kutokana na tendo la kukamatwa na kushitakiwa kwa nia ovu na shilingi milioni 30 kwa kudhalilishwa utu wake.
Ntonge kupitia kwa wakili wake Kelvin Kayaga alidai kuwa siku hiyo Komanya akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Tabora akiwa ameambatana na askari wa jeshi la polisi walifika nyumbani kwa mdai eneo la Ipuli na kumkamata na kisha kumdhalilisha.
Aliongeza kuwa Komamya akiwa na askali wawili wenye Bunduki aina ya Smg baada ya kumkamata walimdhalilisha mbele ya familia yake na majirani ikiwa ni pamoja na kumwamuru apige magoti barabarani.