Na Lucas Raphael,Tabora
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Sikonge mkoani Tabora imehukumu Ngasa Polepole (19) kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana hatia ya kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 4
Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi Mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Sikonge Irene Lyatuu alisema kwamba adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye nia ovu kama alivyotenda kijana huyo bila kuzingatia utu wa binadamu .
Alisema kwamba mahakama imepitia ushahidi wa pande zote mbili ambapo upande wa Jamhuri ulikuwa na mashahidi sita huku mshitakiwa akisimama mwenyewe kwenye utetezi,imejiridhisha pasipokuwa na shaka yoyote
Hakimu huyo mkazi Mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Sikonge Irene alisema kwamba mshitakiwa Ngasa Polepole amehusika moja kwa moja kutenda kosa hilo la udhalilishaji kwa mtoto wa miaka minne ambaye jina limehifadhiwa.
Katika shauri hilo namba 13 la mwaka 2023 alimpa jina la bandia HK kwa lengo la kumlindia heshima muathiriwa wa tukio hilo alisema alichukuliwa na mshitakiwa akiwa na watoto wenzake wawili akawapeleka porini kwenda kutafuta matunda pori ndipo alipofika huko akatenda tukio hilo huku wenzake wakishuhudia dhahiri.
Awali upande wa Jamhuri ukiongozwa na wakili Joseph Mwambwalulu aliiambia mahakama hiyo kwamba mshitakiwa Ngasa Polepole(19) mkazi wa Kijiji cha Madoletisa alitenda kosa hilo majira ya mchana kinyume na kifungu cha 154,hivyo akaiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine .
Hata hivyo waili huyo aliambia mahakama kwamba mshitakiwa ana kumbukumbu ya kufanya makosa mengine ya jinai .
Hata hivyo mahakamani ilitoa adhabu ya kifungo cha maisha na kumtaka mshitakiwa anaeza kukata rufaa iwapo haukuridhika na maamuzi hayo ya mahakama.
Wakati huo huo Mahakama ya hakimu mkazi Sikonge imeahirisha kutoa uamuzi katika shauri la ubakaji linalomkabili Afisa Muuguzi wa hospitali ya wilaya ya Sikonge anayetuhumiwa kumbaka Mama mjamzito ambapo mahakama imepanga kutoa uamuzi katika shauri hilo ifikapo Agost 15 mwa