Wataalamu wa magonjwa ya moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao Suhail Bukhari kutoka Hospitali ya BLK iliyopo nchini India wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu ya miguu (Peripheral Interventions) ambayo haipitishi damu vizuri wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu hayo inayofanyika jijini Dar es Salaam. Jumla ya wagonjwa 70 wenye matatizo ya mishipa ya damu ya miguu iliyoziba wanatarajia kupatiwa matibabu katika kambi hiyo ambayo ni ya kwanza kufanyika hapa nchini
Picha na: JKCI