Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus akizungumza katika Mkutano wa Wajumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai pamoja na Wahariri, Ikulu Jijini Dar es Salam tarehe 20 Julai, 2023.
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Balozi Ombeni Yohana Sefue akizungumza kwenye Mkutano wa Tume hiyo pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.
Mjumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai Ndugu Omar Issa akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali katika Mkutano wa Tume hiyo pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.
Mjumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza katika Mkutano wa Tume hiyo pamoja na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye pia ni Mjumbe wa Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akitolea ufafanuzi masuala mbalimbali ya kisheria katika Mkutano kati ya Tume hiyo na Wahariri kutoka Vyombo mbalimbali vya Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.
Picha zikionesha wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya Habari nchini wakiwa kwenye Mkutano kati yao na Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuimarisha Taasisi za Haki Jinai, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Julai, 2023.
………………………………
Tume iliyoundwa na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan ya kuangalia namna ya kuboresha taasisi za haki jinai, imesema maboresho iliyoyapendekeza kuhusu jeshi la polisi nchini, yamelenga kuliboresha jeshi hilo na sio kulidhoofisha.
Kauli hiyo imetolewa leo Ikulu jijini Dar es salaam na makamu mwenyekiti wa tume hiyo Katibu Mkuu kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue alipokua akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Akifafanua amesema katika mapendekezo yao wamelenga jeshi hilo liboreshe muundo wake ambao utaendana na mahitaji ya sasa ya dunia.
Pia Balozi Sefue amesema mapendekezo yao yataliwezesha Jeshi la Polisi nchini kuwa na chuo cha kisasa ambacho kitazalisha watu wenye utaalamu ambao watakabiliana na uhalifu wa kisasa.
Kuhusu mapendekezo ya kuondoa nguvu ya kisheria kwa wakuu wa mikoa na wilaya ya kumuweka mtu ndani, mwanasheria mkuu wa serikali Eliezer Feleshi, amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kufuata matakwa yote kuhusu sheria hiyo kama inavyotaka,na sio kuikiuka.