Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Dk. Jabir Bakari,akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 18,2023 jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaya hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imetajwa kuendelea kushika nafasi ya kwanza kwa bei ndogo ya data kwa GB 1 ukilinganisha na nchi zote zilizopo katika Nchi za Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
Hayo yamesemwa leo Julai 18,2023 Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA), Dk. Jabir Bakari wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaya hiyo na mwelekeo wa utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2023/2024.
“Hadi kufikia Juni 2023, Tanzania imeendelea kuwa nchi yenye kiwango kidogo sana cha bei ya data kwa GB 1 ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika Mashariki (Burundi, Kenya, Rwanda, Uganda, DRC, South Sudan na Tanzania), ambapo gharama ya 1 GB ni Dola za Marekani 0.71 sawa na Shilingi za Kitanzania 1,666,”amesema Dkt.Bkari
Aidha, amefafanua kuwa mwenendo wa gharama za rejareja za data bila kifurushi na kwenye kifurushi kuanzia mwaka 2015 hadi Juni 2023 (ikijumuisha kodi) zimeendelea kupungua na kuongeza utumiaji wa huduma za Intaneti nchini.
”Tanzania pia inashika nafasi ya saba kwa kuwa na bei ndogo ya data kwa Afrika hii ni kwa mujibu wa Takwimu zilizochapishwa katika tovuti ya Statista na katika Bara la Afrika, takwimu hizo zinaonyesha kuwa wastani wa gharama ya 1 GB ni Dola za Marekani 3.51 hii ni sawa na sh. 8,157.”amesema
Aidha amesema kuwa TCRA kupitia Mfumo wake wa Usimamizi wa simu za ndani na kimataifa imebaini idadi ya dakika za simu za kimataifa zinazoingia nchini kupungua kutoka dakika 3,136,692 mwezi Julai 2022 hadi kufikia 2,900,165 mwezi Juni 2023 sawa na asilimia 7.54.
Amefafanua kuwa kupungua kwa simu za kimataifa kunasababishwa na mabadiliko ya teknolojia na upatikanaji wa chaguzi mbadala za kupiga simu kupitia mitandao ya intaneti kama vile Whatsap, Facebook, Telegram, Zoom nakadhalika.
“Idadi ya dakika za simu za kitaifa ndani ya mtandao mmoja (onnet) zimeongezekakutoka dakika 6,172,696,579 mwezi Julai 2022 hadi dakika 7,012,574,045 mwezi Juni 2023ambayo ni sawa na13.61% hivyo hivyo idadi ya dakika za simu za kitaifa nje ya mtandao mmoja (offnet) zimeongezeka kutoka dakika4,879,102,325 mwezi Julai 2022 hadi kufikia dakika 5,064,800,480 kufikia mwezi Juni 2023 ambayo nisawa na 3.81%,”amesema
Amesema ongezeko la simu za kitaifa linasababishwa na ukuaji wa sekta ya mawasiliano nchini na kwamba katika Kubaini simu za ulaghai TCRA imeendelea kubaini simu za ulaghai zinazoingia hapa nchini na hatua stahiki zimekuwa zikichukuliwa.
” Kutokana na hatua hiyo, idadi ya simu za udanganyifu imeendelea kupungua kuanzia mwaka 2020 hadi Juni 2023, tulibaini matukio machache ya simu za ulaghai yalitokea,katika kipindi cha kuanzia Julai 2022 mpaka Juni 2023, TCRA imeendelea kuwasimamia watoa huduma za mawasiliano kwa kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa masharti ya leseni zao pamoja na kuzingatia viwango vya ubora ,”amesema Dkt.Bakari
Dk.Bakari pia ameeleza, TCRA imefanya maboresho makubwa ya mifumo ya udhibiti wa Sekta ambapo kwa sasa wamejenga uwezo wakufuatilia ubora wa huduma tukiwa ofisini, ili kuhahikisha watoa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti, utangazaji (Radio na Televisheni) na posta wanatoa huduma kwa ufanisi na kwa kuzingatia ubora.
“Aidha, TCRA ilifanya ufuatiliaji na kuhakikisha utekelezaji wa masharti ya kanuni na sheria katika maeneo ya ukaguzi wa watoa huduma kwa kukaguzi watoa huduma 671 wa simu na intaneti, utangazaji na postaili kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa sheria, kanuni, miongozo na masharti ya leseni,”amefafanua
Amesema kuwa TCRA imetoa maelekezo, onyo, na adhabu kwa watoa huduma waliokutwa na ukiukwaji wa sheria, kanuni, miongozo na masharti ya leseni ikiwa ni pamoja na Upimaji wa Ubora wa hudumaza mitandao ya simu katika mikoa ishirini na nne (24), Tanzania Barana mikoa yote ya Zanzibar na kukutana na watoa huduma za mawasiliano ya simu na intaneti kila robo mwaka kujadili matokeo ya upimaji wa ubora wa mitandao ya simu.
“Upimaji wa hivi karibuni ulifanyika kuanzia mwezi Aprili hadi Juni, 2023 umehusishama kampuni (06) ya simukatika maeneo ya miji saba (07) ambayo ni Kahama, Songwe, Mbeya, Kigoma, Katavi, Tabora, and Rukwa. Taarifa za matokeo yaupimaji wa ubora wa huduma za mawasiliano na maendeleo ya sekta zinapatikana kupitia viunganisho vya https://t.ly/nLrwI(Taarifa ya Maendeleo ya Sekta Aprili-Juni 2023) 2.https://t.ly/Hpob6(Matokeo ya Upimaji wa Ubora wa Mawasiliano ya simu Aprili Juni2023),”ameeleza
Hata hivyo amebainisha kuwa katika ukaguzi wa masafa,TCRA hutekeleza ukaguzi huo kila robo mwaka kujua kiwango cha matumizi ya masafa iliyoyagawa kwa watoa huduma nchi nzima na kuhakikisha hakuna muingiliano wa masafa.
Pia amesema kuwa TCRA imeendelea kutatua changamoto za muingilianowa masafa zilizoletwa na watoahuduma na zilizoonekana wakati wa upimaji kama vile muingiliano wa masafa yanayotumika kwa huduma za mawasiliano ya ndege ili kuhakikisha usalama kwa huduma hiyo, muingiliano katika masafa ya radio ili kuhakikisha ubora wa usikivu na muingiliano wa masafa ya simu ili kuboresha huduma za simu.
“Tunafanya pia Ufuatiliaji wa maudhuiya Redio na Televisheni,TCRA imekuwa inafanya ufuatiliaji wa maudhui ya redio na televishenikuhakikisha watoa huduma wanarusha maudhui yanayoendana na sheria, kanuni na miongozo ya utangazaji,katika hili Watoa huduma 152 walikutwa na makosa ya urushwaji wa maudhui yasiyofaa na hatua zimechukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kupewa onyo, adhabu au maelekezo kwa mujibu wa sheria,”amesema Dk.Bakari
Kuhusu upimaji wa Mionzi ya masafa ya rediona simu Dkt.Bakari amesema kuwa TCRA imefanya upimaji wa kiwango cha mionzi ya masafa ya redio na simu kwa mikoa kumi na tano (15) Tanzania ili kuwalinda watumiaji wa huduma za mawasiliano na wananchi wanaoishi karibu na miundombinu ya minara ya Simu, Redio na Televisheni.
Amesema upimaji wa vipimo hivi vilifanyika katika bandi mbalimbali zinazotumika kutoa huduma za mawasiliano ya Simu, Redio na Televisheni na matokeo yalikuwa ni kiwango cha juu katika bandi ya FM Radio (87.5-108 MHZ) kiwango kilikuwa 4.986 V/m (Volt per Meter)ambacho ni chini ya kiwango cha juu kama ilivyoelekezwa na International Commission on Non-Ionizing Radiation Protection (ICNIRP) ambacho ni 27.7 V/m.
“Katika bandi ya ya matangazo ya television (TV UHF (DTT) -470 –694 MHZ) kiwango kilikuwa 4.928 V/m (Volt per Meter)ambacho ni chini ya www.tcra.go.tz asilimali masafa kwa Intaneti ya Kasi TCRA pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kiusimamiziimetoa rasilimali masafa katika bendi za 700MHz, 2300MHz, 2600MHz na 3500MHz yanayowezesha intaneti ya kasi ya4G na5G. Kuwepo kwa Intaneti ya kasi kunawezesha uchumi wa kidijiti katika maeneo mbalimbali kama vile Huduma
za kifedha, utalii, kilimo na huduma za afya,”
Aidha ameeleza kuwa TCRA ipo katika hatua za awali za kufungua bendi za masafa ambazo zitatumiwa na watoa huduma bure bila kuhitaji kuwa na leseni ya rasilimali masafa ili kuuboresha zaidi miundombinu ya Mawasiliano..