Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, akizungumza wakati wa Mkutano wa 6 wa Wataalamu wa masuala ya Fedha, Mipango ya Kiuchumi na Ushirikiano, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, uliofanyika jijini Nairobi, nchini Kenya. Kikao hicho kimelenga kutoa fursa kwa nchi za Kiafrika ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi za muda mfupi na kuweka mikakati ya muda mrefu ya kushughulikia vikwazo vya kimuundo ambapo itasaidia kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuharakisha maendeleo.
Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (kushoto), akisikiliza ajenda mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa Mkutano wa 6 wa Wataalamu wa masuala ya Fedha, Mipango ya Kiuchumi na Ushirikiano, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, uliolenga kutoa fursa kwa nchi za Kiafrika ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi za muda mfupi na kuweka mikakati ya muda mrefu ya kushughulikia vikwazo vya kimuundo ambapo itasaidia kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuharakisha maendeleo, uliofanyika jijini Nairobi, nchini Kenya. Katikati ni Mchumi Mwandamizi wa Wizara hiyo Bi. Glory Sindilo.
Baadhi ya Wataalamu wa masuala ya Fedha, Mipango ya Kiuchumi na Ushirikiano wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika -AU, wakifuatilia Mkutano wa 6 wa wataalamu hao, uliolenga kutoa fursa kwa nchi za Kiafrika ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi za muda mfupi na kuweka mikakati ya muda mrefu ya kushughulikia vikwazo vya kimuundo ambapo itasaidia kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuharakisha maendeleo. Mkutano huo umefanyika jijini Nairobi, nchini Kenya.
Wataalamu mbalimbali wa masuala ya Fedha, Mipango ya Kiuchumi na Ushirikiano wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika -AU, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa Sehemu ya kwanza ya Mkutano wao wa 6, uliolenga kutoa fursa kwa nchi za Kiafrika ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi za muda mfupi na kuweka mikakati ya muda mrefu ya kushughulikia vikwazo vya kimuundo ambapo itasaidia kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuharakisha maendeleo. Mkutano huo umefanyika jijini Nairobi, nchini Kenya.
Na. Joseph Mahumi, Nairobi.
Naibu Katibu Mkuu – Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameongoza ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 6 wa Wataalamu wa masuala ya Fedha, Mipango ya Kiuchumi na Ushirikiano, kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Kikao hicho kinafanyika tarehe 17 hadi 19 Julai 2023, katika ukumbi wa hoteli ya Movenpick, jijini Nairobi, nchini Kenya.
Kikao hicho kimelenga kutoa fursa kwa nchi za Kiafrika ili kukabiliana na changamoto za kiuchumi za muda mfupi na kuweka mikakati ya muda mrefu ya kushughulikia vikwazo vya kimuundo ambapo itasaidia kuimarisha ukuaji wa uchumi na kuharakisha maendeleo.
Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao mbalimbali ambavyo Serikali ya Tanzania imekua ikishiriki ili kutafuta fursa mbalimbali zitakazosaidia ukuaji wa uchumi imara wa nchi.