Na John Walter- Manyara
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Manyara Yustina Rahhi ameishauri Serikali iongeze kasi kupeleka huduma za kijamii maeneo ya Vijijini ili Mazingira yafanane vijana waache kukimbilia Mijini.
Amezitaja baadhi ya huduma hizo ni pamoja na Umeme, miundombinu ya shule,bara bara,maji na Afya.
Amesema kwa kuwa ardhi haiongezeki hivyo serikali ijipange kutoa elimu zaidi kwa Wananchi namna Bora ya kutumia kwa usahihi ardhi iliyopo bila migogoro.
Ametoa ushauri huo katika Mafunzo ya matumizi ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 iliyofanyika leo Julai 17,2023 katika Mji wa Babati mkoani Manyara.
Amesema uwepo wa idadi Kubwa ya vijana maeneo ya miji kumeongeza idadi Kubwa ya wategemezi na kupoteza nguvu kazi ya Taifa kwa kuwa wengi wao wamekuwa wakijiingiza kwenye magenge ya uhalifu na matumizi ya dawa za kulevya.
Kamisaa wa Sensa ya watu na makazi mwaka 2022 Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda, amesema wapo tegemezi halali wanaoanzia umri wa miaka 5-18 na wenye miaka kuanzia 65 na kuendelea hao serikali iwatazame na kuwahudumia lakini wenye miaka 18 na kuendelea na wana uwezo wa kufanya kazi wawajibike kuondokana na utegemezi kwa kufanya kazi Kwa kuwa zipo fursa nyingi.
Amepongeza kuwa wasomi wengi baada ya kuhitimu vyuo ndo wanaongoza kukaa kwenye vijiwe na kusubiri kuhudumiwa na Wazazi wao na kulalamika hakuna ajira.
“Kuongezeka watu ni neema lakini kuongezeka bila kujishughulisha ni mzigo”