Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nzugilo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao katika Kijiji hicho, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Nzugilo wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati ziara yake ya kikazi katika kijiji hicho, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa ambaye pia ni Diwani wa Mpwapwa Mjini, Mhe. George Fuime akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Nzugilo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Mwenyekeiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, ambaye pia ni Diwani wa Mpwapwa Mjini, Mhe. George Fuime (mwenye koti jekundu mstari wa nyuma) akiimba pamoja na Madiwani wa Jimbo la Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene na wananchi wa Kijiji cha Nzugilo uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Idodoma wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao katika Kijiji hicho, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Idodoma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji hicho, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkaoni Dodoma uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipokea taarifa ya Kijiji cha Idodoma kutoka kwa Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Bw. Hashimu Kolezani wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Kijiji hicho uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akifuatilia taarifa ya Kijiji cha Idodoma iliyowasilishwa na Afisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Bw. Hashimu Kolezani kabla ya kuzungumza na wanakijiji wa kijiji hicho kwa lengo la kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na mwananchi wa Kijiji cha Idodoma wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Malolo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi hao katika Kijiji hicho, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akigawa jezi kwa vijana wa Kijiji cha Malolo mara baada ya mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji hicho uliolenga kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo hilo la Kibakwe analoliongoza.
Na Mwandishi wetu-Kibakwe
Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amesema mradi wa umeme katika Kata ya Malolo umefikia asilimia 80 ya ukamilishwaji huku akisisitiza kuwa ifikapo Mwezi Disemba mwaka huu, mradi huo utakuwa umekamilika kwa asilimia 100.
Mhe. Simbachawene ameyasema hayo kwa nyakati tofauti katika Vijiji vya Kata ya Malolo ambavyo ni Nzugilo, Idodoma na Malolo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma kupitia mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa lengo la kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, Ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kikazi za kijiji kwa kijiji kwa ajili ya kuzungumza na wanachi wa Jimbo analoliongoza.
Mhe. Simbachawene amesema hatua hiyo ya kuhakikisha vijjiji vyote vya Kata ya Malolo vinakuwa na umeme, ni utekelezaji wa Ilani ya CCM huku akisisitiza kuwa ni moja ya ahadi aliyoitoa wakati alipokuwa akiomba kura mwaka 2020.
Amesema madai hayo ya wananchi wa Kata ya Malolo ni ya muda mrefu hivyo, anatamani ifikapo mwezi Disemba mwaka huu wananchi hao waache kutumia vibatari, waanze kutumia umeme.
Mbunge huyo ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha kwa ajili ya mradi wa umeme ambao utapelekwa katika vijiji vyote ndani ya Kata hiyo.
Kufuatia hatua hiyo, Mhe. Simbachawene amewasihi Wananchi wa Kata hiyo kuendelea kumuunga Mkono na kumuombea kwa Mwenyezi Mungu, Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili azidi kuwaletea miradi mingi zaidi ya kimaendeleo.
Mhe. Simbachwene ameongeza kuwa, mradi huo wa umeme ambao tayari nguzo zimeshawekwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM, hivyo amewasihi wana Malolo pamoja na kumuunga mkono Mhe. Rais, waendelee pia kumuunga mkono yeye kama Mbunge wao pamoja na Diwani wao Mhe. Dismas Lyao.
“Rais wetu anatupenda sana Wananchi wa Kata ya Malolo ndio maana anataka vijiji vyote vipatiwe umeme hivyo, sisi kazi yetu ni moja tu, kumuunga mkono Mama yetu” amesisitiza Mhe. Simbachawene.
Amesema kukamilika kwa umeme huo kutachochea shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo cha umwagiliaji ambapo kwa sasa wananchi wa Kata hiyo wamekuwa wakitumia majenereta kusuma maji katika umwagiliaji huo ambao ni gharama sana ukilinganisha na umeme halisi.
Awali, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mpwapwa Mjini, Mhe. George Fuime alitumia fursa hiyo kumshukuru Mbunge Simbachawene kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wa Kata ya Malolo huku akimhakikishia kuwa Halmashauri anayoiongoza pamoja na wananchi wote wa Kata hiyo hawatakuwa kikwazo katika masuala ya maendeleo.